HATIMAYE MCHUNGAJI SAEED ABEIDINI AACHIWA HURU TOKA GEREZANI

Mchungaji Saeed Abeidini ©ACLJ

Hatimaye Mungu amejibu maombi ya wakristo wengi waliochukua muda kumuombea mchungaji Saeed Abedini baada ya kuachiwa huru toka gerezani nchini Iran ambako aliwekwa kizuizini kwa kosa la kuhubiri injili nchini humo miaka takribani minne iliyopita.

Mchungaji Saeed ambaye ni raia wa Marekani lakini mzaliwa wa Iran aliachiwa huru siku ya jumamosi iliyoisha, baada ya kuwepo shinikizo kubwa kutoka kwa serikali ya Marekani, taasisi za haki za binadamu bila kusahau wakristo wakiitaka serikali ya Iran kumwachia huru mchungaji huyo. Ambapo taarifa zinasema mchungaji Abedini aliachiwa huru sambamba na wamarekani wengine watatu ambao nao walifungwa nchini humo.

Kwa upande wa mke wa mchungaji huyo aitwaye Naghmeh ambaye aliongoza kampeni mbalimbali za kuachiwa kwa mumewe bila kuchoka ikiwemo kuongoza maombi ya kufunga, katika tamko lake amesema kuachiwa kwa mumewe ni maombi kujibiwa, na kusema familia iko katika hali ya shukrani na kuwashukuru mamilioni ya watu walioshiriki nao katika maombi katika kuhakikisha mpendwa wao anaachiwa huru, aidha amesema kwasasa wanasubiri mchungaji huyo arudi kujiunga na familia yake. Aidha kuachiwa kwa mchungaji huyo kumekwenda sambamba na makubaliano kati ya serikali hizo mbili kuhusu kuachiwa kwa raia wa Iran waliokuwa kifungoni Marekani vivyo hivyo kwa raia hao wanne akiwemo mchungaji pia kuachiwa huru na Irani.

Mchungaji Saeed Abeidini ambaye alibadili dini kutoka uislamu na kuwa mkristo ni baba wa watoto wawili alihukumiwa kifungo cha miaka nane gerezani kwa kosa la kuhataraisha hali ya usalama nchini Iran (ingawa imetafsiriwa kama kosa la kuhubiri na kutaka kubadilisha watu imani yao ya kiislamu ili wawe wakristo jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi hiyo ya kiislamu ya Iran). Ambapo wakati wa kukamatwa kwake alikuwa nchini humo akijenga kituo cha kusaidia watoto yatima. Familia yake imesema mchungaji Abeidini alifanyiwa mateso na manyanyaso gerezani ili aikatae imani yake mpya ya Kikristo lakini hakuogopa kusema na kusimamia ukweli juu ya Kristo.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.