KIGOMA WALITAKA TAMASHA LA PASAKA

Mwisho wa reli, Kigoma. ©Mapio
Na Mwandishi Wetu

Wadau wa Tamasha la Pasaka mkoa wa Kigoma wameonesha nia ya kulitaka Tamasha la Pasaka mwaka huu ili kuepusha vurugu zinazoendelea kwa majirani zao Burundi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi hao wanasema kwa kuwa Tamasha hilo ndio mkombozi wa nchi za Afrika Mashariki hasa kwa masuala ya amani.

Wakazi hao wameiomba Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, kulipeleka tamasha hilo mkoani humo kwa sababu majirani zao nchi ya Burundi wanahitaji uponyaji kutoka kwa waimbaji wa nyimbo za injili na viongozi wa dini.

Burundi imekumbwa na machafuko yaliyotokana na kupinga uongozi wa awamu ya tatu wa rais Pierre Nkurunzinza ambako kila kukicha nchi hiyo inapoteza idadi kubwa ya wakazi wake kwa sababu ya vita.

Ngobho Nyobho mkazi wa Kasulu mkoani humo anasema, tamasha hilo Mkoani Kigoma litakuwa kichocheo cha kuondosha machafuko yanayoendelea nchini humo hasa kwa mauaji ambayo yanawamaliza wananchi wa nchi hiyo kila kukicha.

Mkazi huyo alisema kwa kuwa Tanzania ndio kisiwa cha amani ambayo iliasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambako nchi jirani ambazo zinakosa amani hukimbilia Tanzania kwa lengo la kujiweka sawa.

“Tanzania ni nchi ambayo inasifa kubwa ya kuwa na amani ambayo, nchi zingine zinazoizunguka hakuna, kila kukicha watu wanauana kwa sababu mbalimbali, tunawaomba waandaaji wa Tamasha la Pasaka, kampuni ya Msama Promotions kulifikisha mkoani kwetu kwa sababu ya kuwaomba jirani zao kuacha vita inayoendelea,” alisema.

Naye Ndinda Mahiri mkazi wa Kiganza mkoani humo alisema jirani zetu wanahiaji uponyaji kutoka kwa waimbaji wa Injili na viongozi wengine wa dini na wakemee machafuko yanayoendelea kwa jirani zetu.

Mkazi huyo alisema Kampuni ya Msama Promotions iwafikirie na wao kwa sababu wako karibu na Burundi ambako kuna machafuko yanayoendelea kumaliza idadi kubwa ya wananchi wa nchi hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alisema kamati yake imelipokea ombi hiloambako wameahidi kulifanyia kazi ili majirani zetu Bueundi watapata uponyaji kutoka kwa Mungu kupitia waimbaji wa nyimbo za Injili na viongozi wa dini.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.