KINANA ALITAKIA HERI TAMASHA LA PASAKA 2016

Ndugu Kinana ©DewjiBlog.
Na Mwandishi Wetu.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amelitakia heri Tamasha la Pasaka la mwaka huu linaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, ofisini kwake, Lumumba jijini Dar es Salaam, Kinana analitakia heri na fanaka tamasha hilo na kumuomba Mungu aendelee kubariki utulivu na mshikamano kwa Watanzania wote.

Kinana alisema Tamasha la Pasaka lengo lake ni ujenzi wa Taifa letu na kudumisha amani na utulivu tulionao sambamba na jukumu kubwa la kupiga vita umasikini na kuboresha maisha ya Watanzania na kufikia kiwango cha juu cha maendeleo.

Kinana alisema Watanzania tuna wajibu wa kudumisha mshikamano na upendo miongoni mwetu na tuendelee kusaidiana katika kila hali.

“Tamasha la Pasaka mwaka huu liwe ni muongozo wa kudumisha mshikamano na upendo miongoni mwetu ili tuendelee kusaidiana katika kila hali,” alisema Kinana.

Katibu huyo alisema Watanzania tunatakiwa kuzingatia hayo ili sote kuwa pamoja ili tupige hatua stahili na kuondokana na umasikini uliokithiri.

Mwisho
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.