KWA TAARIFA YAKO: JOYOUS WANAPOMUWEKA MTU BENCHI KUTAFUTA UBORA

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Qhubekani Mthethwa


KWA TAARIFA YAKO kama hujui ni kwamba GK ilikuripotia taarifa ya kuondoka ama kumaliza mkataba kwa kijana mwenye uwezo mkubwa wa kupiga gitaa la bass ndani ya Joyous aitwaye Bheka Mthethwa mapema mwaka jana, pia tukakuweka wazi kwamba nafasi yake ilizibwa na mdogo wake wa damu aitwaye Qhubekani Mthethwa ambaye pia inatajwa kuwa anauwezo wa kumiliki gitaa hilo vyema. Hata hivyo pasipo sababu ambazo GK haijazipata au kufahamu ni kwamba kijana huyo hakuweza kuandika historia kwa kuipigia Joyous wakati wa recording yake ya 20 iliyofanyika kwenye uwanja wa Moses Mabhida December mwaka jana.

KWA TAARIFA YAKO bado hajaifahamika kama ni kiwango ndio kilichosababisha kijana huyo kutojumuishwa kwenye kikosi cha wapigaji ama alipatwa na tukio jingine lililomlazimu kukaa pembeni toka wakati wa maandalizi hadi recording yenyewe. Badala yake gitaa la bass limepigwa na kijana mwingine anayesifika vyema miongoni mwa makundi ya injili na waimbaji binafsi nchini humo aitwaye Sipho Mabena, kijana huyu aliweza kushiriki mazoezi toka awali na kufanikiwa kupanda na Joyous jukwaani kurekodi album hiyo ya kihistoria kwa kundi hilo.

Sipho Mabena


KWA TAARIFA YAKO kwa mujibu wa baadhi ya waimbaji wa injili nchini humo ambao walifanikiwa kumuona Mabena jukwaani na Joyous hawakuacha kumpigia chapuo kwamba juhudi zake zilishaonekana mapema ilikuwa wakati tu ufike ili nyota yake ing'are vyema na kwa pamoja wakaonekana kumpongeza kwakutokata tamaa na kufanikiwa kuonwa na Joyous. KWA TAARIFA YAKO kumbuka sio Qhubekani pekee aliyefikwa na tukio la kutoweza kupanda jukwaani kurekodi na kundi hilo, pia kijana Irebolaji aliyemrithi Sabu kwenye ngoma pia hajafanikiwa kukubalika hadi kuachiwa kupiga wakati wa recording ya kundi hilo badala yake alichukuliwa Bafana Sukwene.

KWA TAARIFA YAKO Kama haitoshi kwasasa Joyous wanampiga drum kijana Thato Rapapane
waliyempachika jina la utani last born akikung'uta ngoma (drums) hata kufanikiwa kupanda jukwaani kurekodi nao. Pia hapana shaka unamkumbuka kijana Uyanda aliyekuwa mdogo wa miaka 11 wakati alipotambulishwa katika ukumbi wa ICC Durban na kupiga kidogo wimbo wa Uvalo Lwami wa kwake pastor Jabu, ni kwamba kundi hilo bado lipo na huyo kijana likiendelea kumkuza ili baadae aje awe mpigaji wao kamili. Hata hivyo bado haijawa wazi kama Sipho ataendelea kuwa mpigaji wa Joyous au alialikwa maalumu kwaajili ya kurekodi nao, vilevile kama kijana Qhubekani Mthetwa bado yupo na Joyous au walishaachana naye.

                        Jikumbushe upigaji bass wa Bheka Mthethwa katika Joyous 19
Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa leo, vinginevyo tukutane wiki ijayo...
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.