KWA TAARIFA YAKO: MPIGANAJI WA ISIS AAMUA KUOKOKA BAADA YA MUNGU WAKE KUTAKA KUMPELEKA JEHANAMU

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. KaribuKWA TAARIFA YAKO hapana shaka umeshasikia mengi kuhusu kile kinachoaminika na wengi kwamba waumini wa dini ya kiislamu ambao watapigana hadi kufa kutetea imani yao ikiwezekana hata kuua mtu hasa kumtetea mtume Muhamad basi moja kwa moja watakwenda peponi ambako watapumzika milele na kufaidi ahadi kedekede walizohaidiwa kwa mujibu wa imani yao (Hata hivyo sio waislamu wote wanaokubali hayo kwamba mtume aliagiza ukiua mtu kutetea uislamu utakwenda peponi). Basi KWA TAARIFA YAKO hii leo tunakutaarifu kuhusu na mmoja wa wapiganaji wa jihadi wa kundi lililojizoelea umaruufu sana la ISIS lililopo nchini Syria na Iraq ni kwamba mmoja wa wapiganaji wake aliamua kubadili dini na kumfuata Kristo mara baada ya kufika mbinguni na kutakiwa kwenda motoni kinyume na matarajio yake ya kuingia peponi.


KWA TAARIFA YAKO kwa mujibu wa taarifa zilizowahi kuandikwa na kutangazwa na Aleppo Herald ni kwamba mwanaume mwenye miaka 32 akiwa mpiganaji wa kundi la ISIS alijeruhiwa vibaya kwa risasi mpakani mashariki mwa Syria na kuachwa kufa hapo lakini mmoja kati ya wamisionari wa Kikristo kutoka eneo hilo alipomuona mtu huyo "akijua amekufa" alimua kumbeba ili akamzike Kikristo lakini baada ya kumbeba mtu huyo kwa mwendo wa kilometa kama 26 ndipo mtu huyo kimiujiza alipozinduka kutoka katika mauti ndipo mmisionari huyo alipoamua kutoa taarifa kwa kiongozi wake aitwaye Hermann Groschlin wote wakiwa katika kundi la Saint Dominican Catholic Presbytery of Ayyash masaa baada ya tukio hilo.


KWA TAARIFA YAKO kwa mujibu wa mtu huyo alisema mpiganaji huyo alimwambia mmishenari huyo kwamba kila siku alifundishwa kufia dini kutamfungulia geti la peponi, na alipokufa (mda masaa machache yaliyopita) alifika mbinguni ambako anasema wakati akielekea kwenye mwanga wa mbinguni ama peponi kama alivyosema mara akatokea shetani aliyemwelekeza njia ya kuzimuni ambako anasema aliweza kuona matatizo na uchangu aliowasababishia watu wengine sambamba na vifo alivyovisababisha kwa watu toka akiwa mdogo, ikiwa pamoja na kujionea namna alivyotenda kwa macho yake Kwa mujibu wa Groschlin amesema vitendo vya kijihadi alivyofanya mtu huyo vitaendelea kumuandama maishani maisha yake yote.


KWA TAARIFA YAKO mpiganaji huyo amedai kwamba kisha Allah ama Mungu kwa mujibu wake amesema alizungumza naye na kumwambia aliishi maisha mabaya sana na kwamba hataruhusiwa kuingia geti la mbinguni kama atachagua kufa, lakini endapo akitaka kuishi tena basi atakuwa na nafasi ya kutubu dhambi zake zote na kuishi njia njema za kumpendeza Mungu jambo ambalo alikubaliana nalo na ndipo aliporudishwa duniani na kuamua kuokoka na kuwa Mkristo siku chache baadae na kudai kwamba aliishi maisha ya kudanganywa awali kuhusu dini na imani yake kuhusu Mungu. Mpiganaji huyo ambaye pia inadaiwa majeraha yake yalipona haraka kuliko ilivyotarajiwa ameamua kujiunga na kikundi hicho cha Kikatoliki huku akimini kwamba habari yake itafanyika msaada kwa wapiganaji wa kundi la ISIS na kubadilisha njia zao na kumrudia Mungu wa kweli.

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kama SPEISA ilivyoripoti, vinginevyo tukutane wiki ijayo....Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.