KWA TAARIFA YAKO : MTOTO WA ASKOFU ANAYEVUMA KANISA JINGINE BAADA YA KUHAMA KWA WAZAZI WAKE

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
KWA TAARIFA YAKO hii leo tunakujulisha kwa ufupi kati ya watoto wa watumishi waliobarikiwa vipaji mbalimbali hususani muziki lakini licha ya baraka za vipawa walivyonavyo, hawavitumii kwenye huduma za wazazi wao badala yake wanavuma sehemu nyingine. Mmoja kati ya watoto hao ambao hata hivyo kwa upande wake alipata ruhusa na uhuru kutoka kwa wazazi wake ni kijana aitwaye Freddy Washington Junior ambaye ni kiongozi wa sifa, mwalimu, mtunzi wa nyimbo, mpigaji wa takribani vyombo vya aina zote akitumika katika kwaya maarufu yenye tuzo kemkem duniani ya The Brooklyn Tabernacle ya jijini New York nchini Marekani.

KWA TAARIFA YAKO Freddy ni mtoto wa askofu Freddy Washington (wana majina sawa ila yeye mtoto anaitwa junior) ambaye licha ya kuwa ni askofu pia anasifa ya kuwa mwimbaji na mpigaji mzuri sana wa vyombo ujuzi ambao hapana shaka amemrithisha kijana wake ambaye pia amesomea masuala ya muziki katika moja ya vyuo hapo jijini New York Marekani. Wazazi wake Freddy wanaendesha huduma yao huko New Jersey Marekani. Kama nilivyoandika awali, Freddy ni kijana mwenye kipaji cha hali ya juu, kipaji chake kinaweza kuonekana kwenye album mpya iliyotoka mapema mwaka jana ya kwaya hii maarufu ya The Brooklyn Tabernacle iitwayo "PRAY" ameshiriki katika utunzi wa nyimbo 12 kati ya 14 za album nzima. Kama haitoshi pia ameanzisha ama amesolo nyimbo tano katika album hiyo.

Bishop Freddy na Pam Washington wazazi wa Freddy

KWA TAARIFA YAKO usipomuona Freddy akiimbisha ama akiimba kwenye kwaya basi tazama kwenye benchi la wanamuziki utamkuta akipiga kinanda huko na tabasamu kubwa. Licha ya kuwa na kwaya hiyo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa, pia kijana huyu ameshatajwa kwenye tuzo kubwa kama za Grammy, Dove na Stellar zote zinatayarishwa nchini Marekani, ambapo pia licha ya kutoa album yake binafsi lakini pia ameshirikishwa na waimbaji wengine. Watu wengi waliosikiliza album yake walikiri kwamba kijana anauwezo na muziki wake ni waviwango vya hali ya juu.

KWA TAARIFA YAKO Unaweza kumsikiliza kupitia wimbo Jesus unapatikana Youtube ama nyimbo nyingine alizoimba na kwaya yake ya The Brooklyn, ambapo kwaya hiyo ilitarajiwa kutoa DVD yake mwaka jana October kama ilivyosema lakini haijatokea hivyo bado watu wanaendelea kusubiri DVD hiyo ambayo wameweka nyimbo mbili tu Youtube kuwapatia wapenzi wao album itakavyokuwa. Licha ya kuongoza sifa katika kwaya kubwa ya The Brooklyn pia Freddy anaongoza sifa kwa upande wa vijana wa kanisa hilo sambamba na kwaya ya watu wachache ambao husafiri na mchungaji kiongozi wa kanisa hilo endapo wanapata mwaliko iitwayo The Brooklyn Tabernacle Singers, kwakuwa kwaya kubwa haiwezi kusafiri umbali mrefu kwasababu ya ukubwa, watu zaidi ya 250. Kumbuka pia kwaya hii ndio iliyokuwa kwaya rasmi katika kuimba wakati wa kuapishwa kwa Rais Barack Obama muhula wa pili.


The Brooklyn Tabernacle Choir wakati wa "Pray" DVD & CD live recording

Tazama  "At the Cross" uliopo katika DVD mpya ambayo haijatoka ukiongozwa na Freddy

    Freddy akianzisha wimbo "The Great I am" wakati wa ibada ya kawaida kanisani Brooklyn

Freddy akianzisha "Every Praise" utunzi wa Ezekiah Walker, ibadani kanisani Brooklyn TBShare on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.