MAKALA: KAZI YA USAMBAZAJI NA VILIO VYAKE

John Maulid,
GK Staff writer.

Nakala ya CD ©wikimedia

Kurekodi nyimbo yaweza kuwa kitu chepesi, na hata kurekodi video pia. Lakini shughuli huanza hasa pale unapokuwa na kazi yako mkononi kisha hujui uanzie wapi ili iwafikie wapenzi wa muziki wa injili.

Kwa vilio hivi nimeguswa kuwashauri na pia kuwafungua wale waimbaji wasiojua chochote katika tasnia hii ya muziki wa injili hasa kuhusu kusambaziwa kazi zao. Waimbaji wengi wanalia na wasambazaji, kila mmoja analia kimpango wake; hii mimi inaniumiza kwakweli unakuta mtu ana nyimbo nzuri lakini inakataliwa lakini unakuta kuna mwingine ameimba “vibaya” albam yake ikachukuliwa. Wewe uliyekataliwa wala usijilaumu wala kujilaumu kwamba una mkosi.

Kuna kitu kinaitwa tamaa, na tamaa humshinda binadamu asiye na hofu ya Mungu.

Kuna watu wamepewa kibali cha kusikiliza kazi ya muimbaji kama ipo vizuri ipitishwe na kusambazwa. Sasa ile nafasi unakuta mtu anaitumia vibaya anataka umpe pesa ili kazi yako isambazwe. Kwa muimbaji asiye jiamini anakubali kutoa hongo halafu unakuta albam inafanya vizuri madukani lakini yeye mwenyewe hana chochote. Hicho ndicho kinachowaumiza waimbaji wengi.

Kingine, kazi nyingi zinaibiwa kutokana na mikataba feki inayofanywa; mathalani unaweza kusaini nakala elfu moja. Hivi kweli kopi elfu moja zinaweza kusambazwa hadi mikoani? Wakati dukani kwake kwenyewe tu unakuta hazitoshi.

Cha ajabu ni kwamba hizo kopi elfu moja Mji wa Dar, na ukienda mikoani napo kila kona nakala zipo. Kwa kweli huwezi Kufikia Malengo yako kwa namna hiyo, pale kazi nyingi zinapoibiwa na wasambazaji.

Kuna baadhi ya wasambazaji unakuta mnasainishana kopi kadhaa halafu hatoi tena na ukivunja nae mkataba unakuta bado anazitoa bila wewe kujua. Wapo wengi wanaofanya michezo ya namna hiyo; kupata msambazaji mwaminifu ni zoezi la kutoa jasho siku hizi. Unaweza kukuta kazi imefika hadi nchi za jirani, lakini imefikaje na wewe labda umesain mkataba wa hapa Tanzania tu.

Wengi hawajui labda niwafungue;

Unapoingia mkataba na msambazaji kuna mikataba miwili; wa ndani ya nchi yako na nchi nyingine, kwa hiyo kama mtasaini wa hapa Tanzania, basi haruhusiwi kuivusha kazi yako nchi nyingine ila wewe unaweza kwenda kuiuza tena labda Kenya au Uganda au nchi nyingine yoyote ile uipendayo.

Pia siku hizi kumezuka mfumo mpya eti kwamba kazi inapopelekwa kwa msambazaji Inabidi producer wa video ammegee yule anaeipitisha kazi Umpe asilimia kidogo ili isambazwe. Na kuna baadhi ya kampuni za kurekodi video zinakubali na kufanya hivyo.

Kikubwa cha kuwashauri waimbaji ni kujiamini na kutotegemea sana soko la Tanzania. Pia wakati nwingine fursa ya kuuza master ikipatikana, uza ili usihangaike na Msabazaji. Lakini pale unapouza master, basi tambua ya kwamba huna haki zozote tena za kuiuza hiyo kazi yako, umeshahamisha umiliki. Ikiendelea kuuza kwa kipindi cha miaka 50, hilo halitokuwa na faida kwako.

Katika haya yote, ni muhimu kumuomba Mungu akuwezeshe kufanya maamuzi sahihi, na hata kuwa na watu bora wa kuisambaza kazi yako. Haleluya!
Share on Google Plus

About John Maulid

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.