MIKOA YAGOMBANIA TAMASHA LA PASAKA 2016

Sipho Makhabane "The Big Fish" kwenye tamasha la pasaka 2013 jijini Dar
Na Mwandishi Wetu

Wananchi wa mikoa mbalimbali wamejitokeza kuiomba kkampuni ya Msama Promotions ianzie Tamasha la Pasaka mikoa kwao mwaka huu huku wakazi wa dare s salaam wakisisitiza libaki mkoani humo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama ameliambia Gazeti hili kuwa, tayari amepokea maombi toka kwa wananchi na mashabiki wa mikoa ya Morogoro, Mwanza, Mbeya, Dodoma na Dar es Salaam wakitaka tamasha hilo lianzie kwao mwaka huu.

“Kamati yangu inafuata taratibu za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambazo ni pamoja na kupata kibali cha kufanikisha kufanyika kwa Tamasha hilo linaloshirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa Injili wa ndani na nje ya Tanzania,” amesema Msama.

Salum Ismail Hamad ambaye ni mdau mkubwa wa Tamasha la Pasaka amesema anawaomba waandaaaji wa Tamasha hilo kutoliondoa jijini Dar es Salaam kwa sababu ni mkoa unaohusisha idadi kubwa ya mashabiki wa muziki wa Injili.

Rukia Joseph wa Kimara Dar es Salaam, alisema yeye anawapigia magoti waandaaji kutoliondoa tamasha hilo jijini Dar es Salaam hasaa kwa waimbaji wa nje ya Tanzania kama Solly Mahlangu na wengineo toka nje ya nchi.

Michael Deogratius alisema ni ngependa Tamasha la Pasaka lihamie mikoani kwa sababu ya ukubwa na umuhimu wa tamasha hilo ambalo linatimiza miaka 16 tangu kuasisiwa kwake.

Msama alisema bado wanasubiri taratibu za kufanikisha tamasha hilo kutoka Basata, hivyo nawaomba wakazi wa mikoani kuvuta subira wakati wakijiandaa.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.