SHANGWE ZA GK: NI ZAMU YA RUTH NA EDSON MWASABWITE


Hayawi hayawi sasa yamekuwa, tarehe 3 Januari ndio siku ambayo historia ya Edson na Ruth imeandikwa kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Kijitonyama na kisha sherehe kufanyika kwenye ukumbi wa Khana Khazana uliopo Victoria Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa mbili hadi saa tano usiku.

Tukio hilo la kipekee liliongozwa na MC Msomi wa sanaa ya mawasiliano, Lawrence Mwantimwa, amabapo pia Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, CHAMUITA, kikiongozwa na Rais wao, Addo November kilikuwepo kuhakikisha kwamba sifa na utukufu zinamrudia Mungu kupitia uimbaji.

Katika hafla hiyo ambayo ilidhaminiwa na Mwanti Car Trade na Gospel Kitaa, Edson Zako Mwasabwite aliimba wimbo maalumu wa kumshukuru Mungu, aliyemuwezesha kufika siku hiyo.

Christopher Mwahangila
Wenyeji, Ruth na Edson
MC Lawrence naye akaimba
Lilian Kimola

Addo NovemberNi kama vile Makondoeko ndiye bodyguard, huku Faraja naye akiwa mpambe wake. Ilipendeza siku hiyo.

Gospel Kitaa inawatakia maisha mema maharusi, waishi katika utukufu wa Mungu.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.