SHANGWE ZA GK: SHEREHE YA SIKU YA KUZALIWA KWA ELIAZER KIMOLA


Siku na masaa zinasonga, na utukufu unazidi kumrudia Mungu. Tarehe 7 ikawa kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa Eliazer Kimola ambaye ametimiza miaka 7 ya kuzaliwa. GK ilifanikiwa kufika na kuungana na watoto wenzake kwa pamoja katika kukamilisha siku hii muhimu lililofanyika KFC Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

Zifuatazo ni picha za tukio;MC King Nyorobi katika kuhakikisha kila kitu kiko sawia.

Mtu na rafikizeKuku ni kwa tumbo


Big bro na madogo

Mama na watoto


Team marekebisho


Kata keki tuleEdna Kuja naye aliambatana na watoto wake.

mahesabu yanapigwa

equation imebalance, kazi na ianze

Sijui kama wanacheza step ama wanfanya mazoezi kabla ya msosi... sijui


Anaitwa Precious KimolaUjumbe kutoka kwa mama yake;

Tarehe 7 January mwaka huooo Mungu alitupa wewe kama zawadi ya mtoto wa kwanza mikononi mwetu. Akatuongoza kukulea na kukutunza tukiwa hatujui kabisa mazoezi haya ya vitendo...
My son ulikuwa kibonge kweli kuliko mimi mama yako wengine hawakuamini kama ni kweli mimi mama yako....ubonge huo ulinifanya mama yako nionekane naweza kweli kulea ki ukweli ni Mungu tu aliyafunika hayo...Leo ni tar 7 ni miaka 7 ulizaliwa jumatano ukazunguka hadi ukaifika hiyo jumatano, maana ya 7 ni utimilifu...na leo ni alhamis umeanza mzunguko mwingine mpya katika maisha yako....Nakupenda sana mwanangu Mungu alikuumba kwa kusudi na tumekuwa tukikuambia mimi na baba yako...uyashike sana mausia yetu mwanangu Eliazer ndipo utaishi miaka mingi na kustawi sana...

Nakupenda mno wewe wajua.....
Happy 7th birthday my son Eliazer!

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.