SITTA ALIBARIKI TAMASHA LA PASAKA

Na Mwandishi wetu,
Samuel Sitta
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, ametoa wito kwa waandaaji wa Tamasha la Pasaka, Kampuni ya Msama Promotions kutosahau kwaya za makanisa mbalimbali.

Kwa mujibu wa Sitta, Msama wanatakiwa wasiweke mkazo kwa waimbaji binafsi pekee bali pia na kwaya za makanisa ambazo mchango wake nao unatambulika.

Sitta pia anampongeza Alex Msama baada ya tamasha hilo kwa namna mapato yake yanavyosaidia makundi yenye uhitaji maalum kama yatima, wajane na walemavu ambao mara nyingi husahaulika.


Sitta amesema matamasha hayo yana malengo mazuri kwa watanzania, hivyo wadau wanatakiwa kumuongezea nguvu katika ufanikishaji wake.

Kwaya za Katoliki, Lutherani, Assemblies of God na nyinginezo sambamba na Kwaya za nje ni muhimu kuwepo ili kubadilishana uzoefu kati ya kwaya za Tanzania na nje.

"Miaka ya hivi karibuni, Kwaya za makanisani tumezisahau, tuzitumie kwa sababu nazo ni eneo letu," anasema Sitta.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ameeleza kuhusu kupokea mawazo ya Sitta ambayo ni ya muhimu, hivyo Kamati ya maandalizi wanayafanyia kazi maombi ya wadau mbalimbali ili kuliboresha zaidi.

Msama alisema hivi sasa wanasubiri kupatikana kwa kibali kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ili kuendelea na taratibu za kufanyika kwa tamasha hilo.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.