SOMO: VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU - MWAL MWAKASEGESEMINA YA NENO LA MUNGU
VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU.
NA MWL MWAKASEGE
ARUSHA MJINI UWANJA WA RELI
TAR 24-JANUARY-2016
DAY 1


Marko 11: 27-28 ‘’ 27Wakafika tena Yerusalemu, wakati Yesu akitembea hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia.
28Wakamwuliza, “UNAFANYA MAMBO HAYA KWA MAMLAKA GANI? Naye ni nani aliyekupa MAMLAKA YA KUFANYA HAYO?
Matendo ya Mitume 4:5-7 ‘’ 5Siku ya pili yake viongozi wa Kiyahudi, wazee na waandishi wa sheria wakakusanyika Yerusalemu, 6walikuwepo Kuhani Mkuu Anasi, Kayafa, Yohana, Iskanda na wengi wa jamaa ya Kuhani Mkuu. 7Wakiisha kuwasimamisha Petro na Yohana katikati yao, wakawauliza, “Ni kwa UWEZO GANI AU KWA JINA LA NANI mmefanya jambo hili?”’’
Yesu aliulizwa swali hili kuwa ni kwa mamlaka ya nani unafanya jambo hili. Hata wanafuzni wa Yesu pia waliulizwa swali hili. Maana kwa akati ule viongozi wa dini hawakujua kuwa walifanya kwa mamlaka ya nani na ni nani aliwepa mamlaka kwa sababu hawakuwahi ona. Maana wangejua wasingeuliza. Pointi ni kuwa si vile vinavyofanyika unapokuwa na mamlaka bali ni VITU GANI vitakuwezesha kutumia mamlaka uliyopewa na Mungu.
MAANA YA MAMLAKA-- ni haki ya kisheria inayompa mtu uwezo wa kuamua na kusimamia utii juu ya kile alichokiamua.
Kwa hiyo kwa kujua maana hii utajua ni kwanini wale viongozi wa dini waliomuuliza Yesu lile swali na walilowauliza akina Petro na wanafunzi ili wajue kuwa ni mamlaka ipi ndiyo waliyokuwa nayo na ni nani aliyesimamia utii wa kile walichofanya maana wakuu wa dini walijua vizuri sana sharia.
LEO TUTAPITIA MAMLAKA AINA 11 AMBAZO YESU AMETUPA.

1. MAMLAKA JUU YA UUMBAJI NA MUNGU.
Mwanzo 1: 24-27 , Mungu katupa mamlaka ya kutawala kila kitu alichokiumba Yeye. Na ona sasa ugomvi wa Musa na Farao na wale waganga na wachawi ulikuwa kwenye viumbe. Ndio maana utaona Musa aligeuza fimbo yake ikawa nyoka na ikameza zingine za wale wachawi. Ivi unajua wachawi wanapigana vita kwa kutumia viumbe mfano Paka, Panya,Nyoka,Mbwa, bundi n.k
Musa alisema kama mimi ni mtumishi wa Mungu na tuone kinachowatokea na ghafla ardi ikafumbua kinywa chake na ikawameza. Yoshua alipojua kuwa maadui zake walikuwa wanapigana nae kutoka kwenye nguvu zilizokuwa kwenye jua na yeye akaamua kulisimamisha jua. Nae Shetani aliamua kutumia mawambi na upepo ili kupigana na Yesu na wanafunzi wa Yesu hawakujua cha kufanya lakini Yesu alijua cha kufanya.

2. MAMLAKA JUU YA PEPO NA MARADHI.
Luka 9:1 ‘’ Yesu akiisha kuwaita wale kumi na wawili pamoja, aliwapa mamalaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote,’’
Kuwa na mamlaka haimaanishi kuwa unaweza kuitumia sawasawa kama Mungu anavyotaka bali kwa hiyo unahitaji sana kuomba sana ili Mungu akupe maarifa vizuri namna ya kutumia mamlaka hii uliyopewa na Mungu.

3. MAMLAKA JUU YA MFUMO WA UTAWALA WA GIZA/ SHETANI.
Waefeso 6:12 ‘’ wamba mweze kuzipinga hila za Shetani. 12Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho’’
Mamlaka ya hapa ni tofauti na ile mamlaka ya kwenye Luka 9:1 , kwa mfano mamlaka juu ya Tanzania na mamlaka ya juu ya watanzania ni tofauti kwa sababu Mamlaka juu ya Tanzania ni juu ya mfumo bali mamalaka juu ya watanzania ni juu ya watu. Kwa hiyo mfano Tanzania kiongozi akifa, watu watahuzunika afu baadae watateua mwingine maana nafasi ile ipo kisheria. Kwa maana hiyo huwezi tumia mamlaka juu ya pepo ili kuja kushughulikia falme. Hizi ni mamlaka unahitaji kujua.

4. MAMLAKA JUU YA UFALME WA MBINGUNI.
Mathayo 16:19 ‘’ 19Nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni na lo lote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, lo lote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.’’
Kwa hiyo jua kuwa mamlaka zina mipaka, kwa hiyo ili jambo lifunguliwa Duniani ndipo linafunguliwa na mbinguni. Lakini order intoka Duniani.
Pia Mungu ametupa kufungua vitu vingine. Kwa hiyo ujio wa Dhambi Duniani iliondoa ufalme wa Mungu. Hata wale waliofungwa na kuzimu unaweza wafungua. Kwa hali hii ni hatari sana kwa Mtu aliyeokoka kutokaa kwenye mamlaka ya ufalme wa Mungu. Hivyo Mungu anaweka watu kwenye mamlaka ili waweze kuzisimamia. Mtu yeyote anapookoka anahamishwa kutoka ufalme wa giza na kuletwa kwenye ufalme wa Mungu.

5. MAMLAKA JUU YA DHAMBI.
Warumi 6:12-14 ‘’ 12Kwa hiyo, msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu, ipatikanayo na kufa, ili kuwafanya mzitii tamaa mbaya. 13Wala msivitoe viungo vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda dhambi, bali jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu Kwake kama vyombo vya haki. 14Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo chini ya sheria, bali chini ya neema.
Warumi 7:15-24 ‘’14Kwa maana tunajua kwamba sheria ni ya kiroho, lakini mimi ni wa kimwili nikiwa nimeuzwa kwenye utumwa wa dhambi. 15Sielewi nitendalo, kwa maana lile ninalotaka kulitenda, silitendi, lakini ninatenda lile ninalolichukia. 16Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, ni kwamba ninakubali kuwa sheria ni njema. 17Lakini, kwa kweli si mimi tena nitendaye lile nisilotaka bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 18Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna jema lo lote likaalo ndani yangu, yaani, katika asili yangu ya dhambi. Kwa kuwa nina shauku ya kutenda lililo jema, lakini siwezi kulitenda. 19Sitendi lile jema nitakalo kutenda bali lile baya nisilolitaka, ndilo nitendalo. 20Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
21Hivyo naiona sheria ikitenda kazi. Ninapotaka kutenda jema, jambo baya liko papo hapo. 22Kwa maana katika utu wangu wa ndani naifurahia sheria ya Mungu. 23Lakini ninaona kuna sheria nyingine inayotenda kazi katika viungo vya mwili wangu inayopigana vita dhidi ya ile sheria ya akili yangu.Sheria hii inanifanya mateka wa ile sheria ya dhambi inayofanya kazi katika viungo vya mwili wangu. 24Ole wangu, mimi maskini! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?.’’
Kwa hiyo tulitegemea hapa Paulo aliposema kuwa Dhambi isitawale maishani mwenu na tulitegema Yeye asiwe na dhambi lakini tunachokiona hapa ni kuwa Pualo anakiri kuwa anadhambi, Kwa hiyo haikukugurantee wewe kuwa na upako kama Paulo na usiwe na dhambi. Na Tafsri ya dhambi ni Uasi lakini hii nayo uhalali wa dhambi kututawala bali sisi tushinde dhambi.

Utajiuliza ni Kitu gani kilikuwa kinamkwamisha Paulo jibu lake ni hili ni MWILI, hata siku moja jaribu kumuuliza Yesu kuwa ni kitu gani kilikuwa kinakukwamisha kwenda msalabani na ulilia sana pale Getsamen atakuambia ni Mwili ndio maana alisema roho I radhi ila mwili ni dhaifu.
Nia na Mwili ni Mauti , maana mwwili hauendi mbinguni na mwili hautiii cha Mungu.
Kwa hiyo ile wewe kuwa na mamlaka juu ya pepo wabaya au maradhi haikupi kibali cha kwenda mbinguni maana Yesu alisema watasema mbona tulitoa unabii, pepo kwa jin lako lakini yeye atawaambia kuwa sikuwajua ninyi. Na ndio maana aliwaambia wanafunzi wake msifurahi kwa kuwa pepo wanawatii bali furahini kwa kuwa majina Yenu yameandikwa mbinguni.
Kwa hiyo mamlaka hizi zinatupa namna ya kutembea hapa Duniani na sio kwenda mbinguni. Suala la kwenda mbinguni ni suala jingine kabisa. Ukiwa na mamlaka iiswe sababu ya wewe kuoandisha mabega na kumsahau Mungu wako.

Lengo la kukuonesha utofauti wa mamlaka hizi ni kujua namna ya kwenda nazo maana kila mlango unafunguo zake maana huwezi tumia funguo za Bedroom ili kufungulia stoo uwe na uhakika hazitafungua.
Yakobo 5:15 Biblia inasema kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii maana maombi kama hayo yanaweza mfungua mgonjwa na kumponya magonjwa yake na kusamehewa dhambi zake. Kwa hiyo unaweza kumuombea Mtu hata kama hana mpango wa kutubu ila kwa sababu wewe umeomb Mungu anamsamehe kabisa.
Ndio maana Mungu anatumia kuhani na kuwaombea watu au kufanya upatanisho na namna ya kufanya toba ili Mungu aje na atengeze hapo mahali ambapo pana dhambi.Unahitaji kujua sana siri hii ya kufanya maombi ambayo yatashughulika na chanzo cha maradhi au magonjwa mabacho ni dhambi.

6: MAMLAKA JUU YA MALANGO YA ADUI.
Mwanzo 22:17 Uzao wako utamiliki malango ya adui. Galatia 3:13,14,29 Biblia inasema amelaaniwa yuke angakue juu ya mti, na Yesu alifanyika laana ili kwa ajili yake ili sisi tupate neema ya kufikiwa na Braka za Ibrahimu ambazo Mungu alituahidi kwa watu wa Duniani kote.

7: MAMLAKA JUU YA MIJI.
Luka 19:16-19 Habari za Yule kabaila au kwa lugha ya sasa tungemwita Mwekezaji na wale watu walipewa yale mafungu ya fedha.
Mafungu 10 alileta faida mara 10 na akapewa mamlaka juu ya miji kumi.
Mafungu 5 alileta faida mara 5 na akapewa mamlaka juu ya miji mitano.
fungu 1 alileta Hakuleta faida yoyote bali alirudisha fedha tu na haikuwa na faida na akinyimwa mamlaka juu ya miji.
Uaminifu juu ya fedha hauleti mamlaka bali uaminifu juu ya matumizi ya fedha ndio unaleta mamlaka juu ya miji.Mwekezaji anaanza kuheshimika kwenye jamii au mji aliopo kwa sababu ya kuwa na fedha. Kwa hiyo hata dini yake nayo inapata sauti kila mtu ataanza kuiheshumu. Usijulize hili ni swala la ulimwengu wa Roho.

8: MAMLAKA JUU YA MIFUMO YA KIUTAWALA YA WANADAMU.
Waefeso 2:6. 6Mungu alitufufua pamoja na Kristo na kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu
Waefeso 1:20-23 20ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamketisha mkono Wake wa kuume katika mbingu, 21juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali na katika ule ujao pia. 22Naye Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya miguu Yake na amemfanya Yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya Kanisa, 23ambalo ndilo mwili Wake, ukamilifu Wake Yeye aliye yote katika yote.
Ufalme wa wadamu umetambulishwa kama NGUVU AU USULTANI lakini vyote ni ufalme wa wanadamu.
Soma Ufunuo 17:1-2

9: MAMLAKA JUU YA MAENEO MUHIMU YENYE MAKUSNYIKO YA WATU.
Ufunuo 5: 9-12 Wanamiliki juu ya
i) Kabila
ii) Lugha
iii) Jamaa/ukoo
iv) Taifa.
Ufunuo 17:15-
Ndio maanampinga kristo anafuatilia juu ya soko yaani kuuza na kununua kila sehemu yeye anafuatilia hasi kwenye mitandao. Soma Ufunuo 13.

10: MAMLAKA JUU YA KILA FIKRA.
2Wakorintho 10:3-5 3Ingawa tunaishi duniani lakini hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. 4Silaha za vita vyetu si za mwili, Bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. 5Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo
Jiulize swali hili je kuna fikra ngapi ambazo hazimtii kristo na je sisi tumechukua hatia gani ili kuzifanya zimtii kristo. Chukua hatua kushughulika na kila fikra isyomtii kristo na iweze kumtii kristo.

11: MAMLAKA JUU YA ULIMI NA KINYWA CHAKO.
Yakobo 3:1-12 Mtu Yupo kama meli, mtu atakula matunda ya kinywa chake. Kwa hiyo hata ndoa nyingi huvunjika kwa sababu ya maneno na hadi hufika hatua ya kusambaratika kabisa.
Ulimi ni Karamu na Roho Mtakatifu ni wino. Kwa hiyo kuwa makini sana na matumizi ya ulimi wako.

Itaendelea Kesho.....
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.