SOMO: VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU - MWAL MWAKASEGESEMINA YA NENO LA MUNGU 
VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU.
NA MWL MWAKASEGE
ARUSHA MJINI UWANJA WA RELI
DAY 2⃣
TAR 25-JANUARY-2016

Kusoma sehemu iliyopita BONYEZA HAPA

📖Marko 11: 27-28 ‘’ 27Wakafika tena Yerusalemu, wakati Yesu akitembea hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia. 28Wakamwuliza, “UNAFANYA MAMBO HAYA KWA MAMLAKA GANI? Naye ni nani aliyekupa MAMLAKA YA KUFANYA HAYO?

📖Matendo ya Mitume 4:5-7 ‘’ 5Siku ya pili yake viongozi wa Kiyahudi, wazee na waandishi wa sheria wakakusanyika Yerusalemu, 6walikuwepo Kuhani Mkuu Anasi, Kayafa, Yohana, Iskanda na wengi wa jamaa ya Kuhani Mkuu. 7Wakiisha kuwasimamisha Petro na Yohana katikati yao, wakawauliza, “Ni kwa UWEZO GANI AU KWA JINA LA NANI mmefanya jambo hili?”’’
Ile kuwa tu na mamlaka haitoshi bali leo nataka tuangalie Zaidi kuwa hizo mamlaka nilizokufundisha jana utazitumiaje.
👇👇
Leo tunaangalie     VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU

Mwanzo 1:28 ‘’ 28Mungu AKAWABARIKI na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia b na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.’
Neno AKAWABARIKIA maana yake ni kuwa akawapa vitu ambavyo vitawawezesha  kufanya yale ambayo Mungu aliwaagiza kufanya. Na ukiangalia vizuri utaona kuwa Mungu aliwabariki kabla ya kuwaingiza kazini au kuwapaagizo la kuwa zaeni mkaongezeke na kuijaza nchi na kuitisha.

KAZI YA BARAKA.
Kazi ya Baraka ni kukuwezesha kuwa kama Mungu anavyotaka uwe au anavyotaka ufanye kama vile yeye anavyotaka.

MAANA YA KUITISHA, ni kumiliki kwa amri au mamalaka hata kama nchi haitaki.
Kwa hiyo msisitizo wa Somo kuwa tu na mamlaka bali ni kujua namna ya kuitumia.

☀POINTI YA 1 . MUNGU AKUPE KUJUA YA KUWA MAMLAKA ALIYOKUPA KATIKA KRISTO NI MAMLAKA AMBAYO CHIMBUKO LAKE NI ULIMWENGU WA ROHO.

Leo natakata twende kwa mifano ili tuweze kuelewana katika somo hili.

Tuangalie mamlaka amabayo Mungu amaetupa katika uumbaji wake

 Mwanzo 1 :24-28  Katika kitabu cha mwanzo utaona uumbaji wa Mungu na Mungu kuwabarikia watu wake. Kumbuka kuwa Mtu ni Roho anayo nafsi anaishi katika mwili.

Na ukisoma katika Mwanzo sura ya 1 na 2, tunaona Sura ya 1 roho ya mwanadamu ikiumbwa na baadae kaika sura ya pili ndio tunoana mwili kuumbwa na kuweka pumzi na kuwa nafsi hai.Hivyo Mwanaume na Mwanamke waliumbwa wote kwenye sura ya kwanza ila miili yao ndio imekuja kuumbwa kwenye sura ya pili.

Suala la Mwanamke ni kuzaa au kutozaa ni sauala la ulimwengu wa roho kabla halijawa suala la kimwili.

☀MFANO: Kuna mwanamke mmoja katika mkoa mmoja nilikukokwa nafanya semina na alikuwa na tatizo la kupata mimba maana kila akipata mimba zinakaa miezi miwili tu na huwa zinatoka. Na yapata mimba kama 6 ivi zilikuwa tayari zimeshatoka. Na akaja na tukaomba Mungu lile tatizo liondoke na kweli baada ya Muda akaja akapata mimba  na hiyo mimba nayo ikatoka. Na alipokuja tena kwangu nikamuuliza kwanini umetoa mimba.

 Akaanza kujitetea kuwa Mwakasege mimi sijatoa mimba imetoka yenyewe, bali mimi nikamuuliza jibu swali kwa nini umetoa mimba. Ilikuwa ni ngumu sana kwa yule mama kunielewa ila nikamuuliza kuwa ivi je maiti huwa inapata mimba. Akasema hapa ni kasema kwa hiyo kipi kinapata mimba ni roho au mwili wako? Na akasema ni roho kwa hiyo nikamuambia ukipata mimba nyingine tena isemeshe kuwa usitoke hadi miezi tisa itakapotimia. Tukaomba nikamuacha.

Baada ya Muda akaja akapata mimba tena na baada ya miezi miwili dalili za kutoka mimba zikaanza tena na akaanza kutatufuta kila mahali na Mungu alituficha kila akija mahali tulipo anatukosa mara utasikia tumeondoka na kwenda mahali pengine. Baada ya kutukosa akarudi kwake na kuanza kusoma yale tuliyomfundisha. Na alipoanza kikiri ile mistari mara ile hali ikakoma na akapata mtoto wa kwanza na wa pili na wa tatu …. Ooh haleluya haleluya.

 Hapa nataka uone jinsi Mungu alivyomfundisha Imani na hakika Mungu alimsaidia. Jifunze sana juu ya kutumia mamlaka ambazo Mungu ametupa.

📖Kutoka 10:21-23 21Kisha BWANA akamwambia Musa, “Nyosha mkono wako kuelekea angani ili giza litande katika nchi ya Misri, giza ambalo watu wanaweza kulipapasa na kulihisi.’’ 22Kwa hiyo Musa akaunyosha mkono wake kuelekea angani, na giza nene likafunika pote katika nchi ya Misri kwa muda wa siku tatu. 23Hakuna mtu ye yote aliyeweza kumwona mwenzake, wala kuondoka mahali alipokuwa kwa muda wa siku tatu. Lakini Wasraeli wote walikuwa na mwanga katika maeneo yao waliyokuwa wanaishi
Hapa tunaona wana wa Israel wakiwa na Nuru na Wamisri wakiwa na giza na ili uelewe vizuri mamlaka hii aliyoitumia Musa kuingilia mfumo wa Nuru inabidi uone kilichoandikwa kwenye kitabu cha

📖 Mwanzo 1:14-15 ‘’ Mungu akasema, “Iwepo mianga kwenye nafasi ya anga ili itenganishe mchana na usiku, nayo iwe alama ya kutambulisha majira mbali mbali, siku na miaka, 15nayo iwe ndiyo mianga kwenye nafasi ya anga itoe nuru juu ya dunia.’’

👉🏼Ikawa hivyo
Kazi ya Jua ni kutawala mchana na mwezi utawale usiku. Lakini Musa alipewa mamlaka ya kuweza kuingilia mfumo wa jua na kukata  mwanga wa wamisri  na kuweka mwanga kwa wana wa Israel.

 Yaani ina maana wamisri walikuwa hata wakiwa na taa zilikuwa hazitoi mwanga. Suala la giza na nuru kabla halijawa suala la kimwili limekuwa suala la kwanza kabisa katika ulimwengu wa roho.

👉🏼Chanzo cha kusoma haya ni kutokana na hali iliyokuwa ikinusumbua sana ya mvua kunyesha kila mahali ukiweka hema hii ya kwetu mvua ilikuwa inaanza kunyesha  au hata me mwenyewe nikenda mahali utakuta mvua tu inaaanza hata kama sio majira yake. Ndio nikaanza kutafuta majibu kwenye biblia.  Na ndipo Mungu aliponifundisha namna ya kuingilia majira na  namna ya kuidhibiti mvua.

☀MFANO WA MOROGORO.

Nakumbuka mwaka mmoja tulikuwa tunaandaa semina ya Morogoro na nikawauliza wenyeji wakasema mvua kwa sasa imeisha na tukapeleka hema na sku ile tunafunga hema mvua kubwa ikawa inanyesha na wenzutu walijenga hema katikati ya mvua na semina nayo ilianza kwenye mvua kama siku tatu ivi mvua ilikuwa inanyesha na watu walikuwa wanakuja wengi na miamvuli. Hapo nikaona sasa hii mvua itatuharibia utaratibu  na utulivu nikaomba Mungu mvua ile iache kunyesha hadi tutakopamaliza semina. Na nilikuwa nakaa kwenye hoteli karibu na milima ya uluguru. Na mvua ikaanza kunyesha milimani nilikuwa nainyoshea kidole kuwa ewe mvua usije huku mjini hadi nimalize semina. Na baada ya hapo unaona wingu linaondoka na mvua inakoma kabisa.


Basi siku ile ya mwisho tunamaliza semina nikawaambia wakazi wa Morogoro kuwa samahani jamani nilimaisha mvua ili tuwe na semina ila kuanzia kesho saa kumi mvua itarudi (baada ya kuwaambia wenzangu kuwa hema litaanuliwa kabla ya saa kumi na kuweka kwenye gari tayari kwa safari). Basi mtu mmoja alisema haya anayoyasema yakitokea me ntaokoka.

Baada ya saa kumaliza semina ile kesho yake tulimtembelea mtu mmoja Morogoro tukawa tunamsalimia na ilipofika saa kumi baada ya kuwasiliana na wenzangu kuwa hema na ila kitu tayari wamepakia kwenye lori la kwetu  na manyunyu ya mvua yakaanza taratibu, na mkwe wangu akanikumbusha kuwa tuliiambia mvua inyeshe kuanzia saa kumi na kuendelea sisi kukaa pale ile tulikuwa tunaizuia ile mvua.

 Basi tukaaga na tulipoanza kuondoka maana tulikuwa tunaenda Dar es Salaam kwa gari. Mvua kubwa ilinyesha Morogoro usiku kucha  na kesh yake ikaendelea kusnyesha na kunyesha. Watu wakampigia simu mwenyekiti wa kamati ya kwetu Morogoro ya kuwa tunaomba Mwambie mwakasege aisimamishe mvua sasa maana inatosha sasa.  Oooh haleluya haleluya…..


Hii ni mamlaka ambayo Mungu anakupa  lazima unajua kuwa ni mamlaka ya ulimwengu wa roho na inahitaji hekima sana kuitumia na usiitumie wewe utakavyo maana utaanza kuleta usumbufu kwa watu wengine.

🎆MAMLAKA JUU YA MFUMO WA SHETANI.
Waefeso 6:12 ‘’ 12Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Waefeso 3:8-11 ’’ 8Ingawa mimi ni mdogo kuliko aliye mdogo kabisa miongoni mwa watakatifu wote, nilipewa neema hii ili niwahubirie watu Mataifa kuhusu utajiri usiopimika ulio ndani ya Kristo na 9kuweka wazi kwa kila mtu jinsi ile siri iliyokuwa imefichwa kwa nyakati zote katika Mungu aliyeumba vitu vyote. 10Ili kwa njia ya Kanisa, hekima yote ya Mungu ipate kujulikana kwa watawala na WENYE MAMLAKA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO, 11SAWASAWA NA KUSUDI LAKE LA MILELE KATIKA KRISTO YESU BWANA WETU. 12YEYE AMBAYE NDANI YAKE NA KWA NJIA YA IMANI KATIKA YEYE TUWEZE KUMKARIBIA MUNGU KWA UJASIRI NA KWA UHURU. 13Kwa hiyo, nawaomba msikate tamaa kwa sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu, hayo ni utukufu wenu.
Kwa hiyo ile kuwa na mamlaka juu ya mfumo wa shetani haitoshi bali inahitajika pia kujua mamlaka juu ya mfuno wa utawala wa wanadamu.

 Angalia Waefeso 1:20 utaona neno katika Ulimwengu wa roho juu sana kuliko falme na mamlaka na kila jina litajwalo. Mungu katuweka juu sana juu ya mamlaka juu ya ufalme wa Shetani na ufalme wa Wanadamu. Hivyo ni muhimu sana kuwa na maarifa ya kushughulika na watu na mifumo yao ya kiutalawa.

🙇🏼MAMLAKA JUU YA KILA FIKRA.
   2Wakorintho 10:3-5  ‘’ 3Ingawa tunaishi duniani lakini hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. 4Silaha za vita vyetu si za mwili, Bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. 5Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo.
Hapa tunaona kuwa hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili bali tunafanya kwa jinsi ya rohoni na tukiangusha mawazo na kila fikra isiyo mtii kristo na ipate kumtii kristo. Na kila kijiinuacho juu ya Elimu ya Mungu nacho kipate kumtii Mungu.
👇👇

Twende kwa Yesu tukawaangalie wanafunzi wawili yaani Yuda na Petro. Yuda alikuwa  ni mpole sana na Petro kwa lugha ya sasa tungesema alikwa na kiherehere sana au msemaji sana. Petro aliposikia habari za Yesu kwenda msalabani alimwita na akaanza kumkemea na kumwambia rudi nyuma ewe shetani kwa sababu huwazi ya Mungu. Yesu alikuwa anamwambia petro umeside/ umeingiliwa na shetani saa ngapi. Bila Yesu kumkemea shetani lile pepo lingeendelea kumsumbua sana Petro. Hii ilitokana na Shetani kuomba kibali kuwa anataka awapepete kama ngano na Yesu akamwambia Petro shetani ameomba kibali ili awapepete kama ngano lakini mimi Yesu nimekuombea ili utakapoongoka uwaimarishe na dnugu zako.

Yesu alipokuwa anazungumza na wanafuzni wake kuwa watamkibia na kumkataa ila Petro alisema mimi sitaweza, Yesu alimwambia kuwa Petro utanikana Mara tatu na Petro alimkana Yesu mara tatu na mara ya  tatu alinaani kabisa. Ina maana alikuwa maejitoa kwenye uanafunzi wa Yesu.

Ndio maana Yesu alipofufuka aliwaambia waambieni wanafunzi wangu na Petro ile neno Na Petro ina maana petro hakuwa mwanafunzi tena. Na ndio maana Yesu alipokuwa nazngumza nao alimwambia Petro mata tatu kuwa je wanipenda, hii ilikuwa ni kumsaidia Petro maan aalimkana Yesu mara tatu.

MFANO. Wangapi hapa wanajua kuendesha baiskeli, 🚲na je unaweza kuacha kuandesha baiskeli, jibu ni hapana. Maana yake ni kuwa kitu kimeingia kwenye mfumo wako wa fahamu na halitoki. Hata kama haumkumbuki aliyekufundisha kuendesha baiskeli ila hautakauja ushahau kuendesha baiskeli.
Kwa hiyo kumkemea pepo tu haitoshi maana huwezi jua kuwa ni kitu gani kaweka kwenye fikra za mu huyo. Hivyo pia kuomba matengenezo kutoka kwa Mungu juu ya mtu ambaye umekea lile pepo limtoke ili mfumo wake wa fikra urudi kama Mungu alivyoagiza.

📖Luka 22:1-6  Hapa tunaona Shetani akimwingia Yuda na kumfanya amsaliti Yesu, na Yuda aliwaambia wakuu wa makuhani kuwa yeye ndiye aliyekuwa karibu sana na Yesu  na akawapa na mbinu za namna ya kumkamata na jinsi atavyofanikisha ndipo akapewa rushwa ya vipande thelathini vya fedha.
Shetani nae alikamata fikra za Yuda hadi hukumu ilipoingia ndani ya Yuda na aksahau hadi kumwamini MUngu ili kuwa anawezakumsamehe maana Mungu anasema dhambi yako ijapokuwa nyekundu kama damu itakuwa nyeupe kama theluji, ila Yuda alisahauna hadi akajinyonga. Hata kama umemkosea Mungu namna gani rudi kwa Mungu na Mungu atakusamehe, usiogope rudi kwa Bwana maana huko  kwingine hakuna msaada na usije fanya maamuzi kama Yuda, Njoo kwa Yesu ndio maana alikufia msalabali rudi rudi kwa Bwana.

👉🏼Elimu ni suala la kiroho kabla halijawa la kimwili na ona maarifa ambayo watu wanapewa baada ya Muda utakuja kuona watu wanaanza kujitenga na Yesu na kuanza kukaa mbali na uso wa Mungu. Kwa hiyo ni muhimu sana kuombea elimu ambazo watu wanapewa ili ziwe za Elimu ya Mungu na sio zingine maana shetani nae ana elimu yake inayomnfanya amkatae Mungu.
Ili kujinaua hapo mahali Fanya maombi ya aina tatu.
👇👇
1: OMBA KWA MUNGU MACHO YAKO YATIWE NURU.
Waefeso1:17-23  ndio maana Paulo aliwaombea watu wa efeso japo walikuwa wameokoka lakini aliwaombea maombi haya. Na mimi ni sala yangu  ya kila siku huwa najiombe maombi haya mara kwa mara.na wewe chukua sala hii ni ya kwako jiombee kila siku  kila siku na iwe ni utaratibu wa maisha yako ya kila siku
👇👇
2: OMBA MUNGU AKUPE KUTAFSIRI KWA JINSI YA ROHONI KWA MANENO YA ROHONI.
1Wakorintho 10:10-14  na Waebrania 11:3 Kwa Imani twafahamu  kuwa ulimwengu uliumbwa kwa vitu visivyooneka, na katika warumi 10:17 imani huja kwa kusikia na katika ulimwengu war oho inatupa kufahamu.
👇👇
3: OMBA MUNGU AKUSAIDIE KUKUA KIROHO.
Wagalatia 4:1-2 Lakini nalisema nanyi kama watoto. Mrithi ajapokuwa mtoto huwa kama mtu hadi pale wakati ule ulioamriwa na Bwana wake. Kwa hiyo lazima ukue kiroho ili ukue kiroho na ndipo vitu vingine utaweza kuvitumia.
Mfano: Ukiwa na mtoto wako mwenye miaka 10 ukamnunulia gari na ukampa kuwa uwe ni urithi wake, hata kama anajua kuendesha sharia ya nchi haimruhusu kuanza kuendesha gari kwa sababu hajatimiza miaka 18. Kwa hiyo ukubwa (ukomavu) ni muhimu sana katika ulimwengu wa roho.

☀Jiombee sana sana maombi haya, na usiseme ntasubiri sema hii iishe ndio nianze kuifanyia kazi. Bali nakushauri anza sasa kuitendea kazi usiache semina hili lipite bure.

Itaendelea kesho..
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.