T.A.G ILALA KUMEPAMBA MOTO KATIKA UZINDUZI WA DVD YA DINA MGOMERA

Leo ni leo, asemaye kesho bado amelala, kwa maana milango ya baraka imeshafunguliwa pale kanisa la Tanzania Assemblies of God Ilala, ambapo Dina Mgomera anazindua DVD yake ye Nina Haja Nawe.

Kabla hata ya saa nane kutimu, makundi ya watu tayari yalikuwa eneo la tukio wakisikilizia tu muda rasmi, huku sauti ya kujaribu usikivu wa vyombo ndio zikipenya masikioni mwao na kuwa tulizo la roho.

Gospel Kitaa ambayo iko eneo la tukio, imeshuhudia nyuso zenye furaha, huku waimbaji kadha wa kadha wakiwa tayari kumrudishia Mungu sifa na utukufu kupitia uimbaji wa kutumia vyombo (live).
Sehemu ya watakaoimba leo ni pamoja na The Jordan Band, One Voice Family International, Bwana Harusi Edson Zako Mwasabwite (bofya kuona harusi yake), na wengine wengi.

Zifuatazo ni picha za awali wakati tamasha likiwa linakaribia kuanza. ambatana nasi.
Furaha Isaya

Kama bado hujajua kinachoendelea basi tazama video ifuatayo;Share on Google Plus

About Bony Kazi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.