TANZIA: MWIMBAJI NYOTA WA MUZIKI WA INJILI NCHINI CONGO AFARIKI DUNIA


Habari ambazo GK imezipata ni kwamba mwimbaji nyota wa muziki wa injili kutoka jamhuri ya Kidemokrasia  Kongo aitwaye Marie Misamu ametwaliwa kutoka dunia hii usiku wa kuamkia leo.

Taarifa za awali zinasema mwimbaji huyo aliyetokea kupendwa nchini humo na hata baadhi ya kazi zake kupatikana nchini Tanzania, alikuwa mgonjwa na kulikuwepo na ombi kutoka kwa bintiye aitwaye Ruth Misamu aliyewataka watu waliokuwa wakiulizia hali ya mwimbaji huyo kuwaomba wamuombee mama yake. Tutakujulisha endapo tutapata taarifa zaidi juu ya kifo chake

                Angalia kati ya kazi za marehemu zinazopatikana Tanzania. (Ee Yahwe)


             BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.