VITUO VYA YATIMA VYALIOMBEA TAMASHA LA PASAKA 2016

Na Mwandishi Wetu
Sehemu ya misaada ambayo hutolewa na kampuni ya Msama Promotions.
Vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima jijini Dar es Salaam vinaliombea Tamasha la Pasaka 2016 kwa sababu Kampuni waaandaaji wa tamasha hilo mara zote huwakumbuka na kuwajali yatima.

Mmiliki wa kitupo cha Mandaliwa kilichopo Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Halima Ramadhani alitumia fursa hiyo kumuombea Mungu muandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama kuliendeleza tamasha hilo na amfungulie njia kila anachokifanya.

Ramadhani alisema Mungu amlinde na fitna za watu ili afanikiwe kwa sababu yatima wanalitegemea sana tamasha hilo ambalo linawasaidia mahitaji mbalimbali.

Mmiliki wa kituo cha Honoratha kilichopo Temeke, Honoratha Michael aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kumsaidia Msama katika kufanikisha tamasha hilo kwa sababu mojawapo ya vipaumbele vya Msama ni kuwasaidia yatima.

Katibu wa kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni Moscow, Rashid Mpinda, anamshukuru Mungu kwa ajili ya Msama kusaidia yatima, na kwamba serikali imsaidie eneo ambalo litakuwa ni muunganiko baina ya yatima na jamii.

“Msama hana utajiri wowote, nawaomba wadau wengine wajitokeze kufanikisha misaada kwa jamii,” alisema Mpinda.

Aidha Mpinda alisema kila kituo chake wanamuombea dua maalum Msama kwa lengo la kufanikisha matakwa ya wenye uhitaji maalum.

Sudi Said wa kituo cha Zaidia kilichopo Sinza Madukani anazidi kuliombea Tamasha la Pasaka kwa sababu linawasaidia hivyo wako pamoja naye katika kufanikisha tamasha hilo.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.