WAIMBAJI WAENDELEA KUMPA SALAMU BAHATI BUKUKU

Sehemu ya waimbaji kwenye msiba wa baba yake Bahati mwaka 2013. (Habari)
Waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili wamemtumia salamu za rambirambi muimbaji mwenzao Bahati Bukuku kufuatia kifo cha mama yake mzazi.

Mmoja kati ya waimbaji hao ni Ambwene Mwasongwe ambaye ametuma salamu hizo kwa njia ya whatsapp baada ya kuweka Profile picha ya Bahati Bukuku na kuandika ujumbe wenye maneno " Mungu akutie nguvu dada! Pole kwa kumpoteza mama"

Muimbaji mwingine ni Bupe Mizeck ambaye ameweke picha kwa whatsapp ambayo wamepiga pamoja na Bahati Bukuku na kuandika "Pole sana Rafiki yangu Bahati Bukuku kwa kufiwa na mama yetu mpenzi mrs Bukuku!! R I P mama!"

Mwaka 2013, Bahati Bukuku alifiwa na baba yake, Mzee Lwaga Bukuku, ambapo waimbaji kadha wa kadha pia walijitokeza kumfariji. (bofya hapa kuona)

Bahati Bukuku ni muimbaji wa siku nyingi wa nyimbo za injli nchini, ambaye amewahi pia kunusurika kifo kwenye ajali ya gari. (bofya hapa kuona)
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.