CHAGUO LA GK: MIGHTY TO SAVE YAKE ANGEL BENARDUhali gani mdau wa Gospel Kitaa kwa Jumapili ya leo, tunatumai Mungu anaendelea kutuwezesha katika yote tunayopitia, maana hakuna kilicho kigumu kwake.

Katika Chaguo la GK wiki hii tunaye mwanadada Angel Benard, na wimbo wake wa Mighty to Save. Mungu wetu ana uwezo wa kuokoa katika kila aina ya dhiki, adha, njaa, ama tatizo liwalo lololte lile. Ndivyo Angel ama Mrs Sakafu anavyotukumbusha kupitia video hii ambayo ameimba live kwenye mkesha wa Campus Night uliofanyika Jijini Arusha mwezi Januari.

GK inakuletea live production ya wimbo huu kutoka mkesha huo.. Uwe na Jumapili yenye baraka tele.
Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.