CHAGUO LA GK NI KUTOKA KWA WANA WA FURAHA GANI TOKA ST JAMES ARUSHAKatika chaguo la GK kwa siku ya leo tupo jijini Arusha kwa mara nyingine, safari hii tunakupa wimbo mzuri uitwao "Sisi tumetenda dhambi" kutoka kwaya kongwe ya Upendo kutoka St. James Kaloleni Arusha ambao wanatambulika zaidi kwa jina la Furaha Gani kutokana na kazi nzuri waliyoifanya kwenye video ya kwanza iliyopewa jina hilo. Wimbo huu tuliokuchagulia unapatikana katika video yao ya pili. Hapana shaka utakubaliana nasi kwamba usharika huu wa St James umebarikiwa kuwa na kwaya nzuri ambazo zinafanyika baraka kwa watu wengi. Tunakutakia utazamaji mzuri na jumapili njema

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.