KIPAJI KINGINE CHAJIENGUA JOYOUS CELEBRATIONHii inawezakana ikawa taarifa mbaya kwa mashabiki wa kundi la Joyous Celebration hususani wapenda muziki wa kundi hilo, baada ya kijana anayesifika kwa upigaji wa piano Jkatika kundi hilo Lungelo Ngcobo kuandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Facebook akiaga kwamba atawakumbuka waimbaji na wapigaji wenzake ambao aliwataja kwa majina baadhi yao na kuwataka waendelee vyema kuponya roho za watu kupitia utumishi wao katika kundi hilo.

Lungelo anakuwa mmoja kati ya wana Joyous waliomaliza mkataba na kundi hilo ili kuendelea na utumishi wao sehemu nyingine katika kipindi kifupi. Ambapo alianza kuonekana katika jukwaa la Joyous kuanzia DVD ya 17 na kuhitimika katika DVD ya 20 ya kundi hilo ambayo inatarajiwa kutoka mapema kabla ya kuzinduliwa rasmi wakati wa pasaka mwaka huu.

    News Feed

    I'm really gonna miss looking at Siyanqoba Mthethwa and Lebo Morolo at the stage !!! Guys I had the most fun with!!!! And as for my favorite vocalists Mnqobi Nxumalo, Phelo Bala , Hlengiwe Ntombela , Londiwe Malondi Masondo , Buhle Thela , Ayanda Shange , may God bless you all and bring more souls through you guys !!!!! Bless you all ‪#‎JoyousCelebration‬
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.