KWA TAARIFA YAKO: KIJANA WA SHEKHE ALIYEAMUA KUMTUMIKIA MUNGU

Abuu kwenye ubatizo wa maji mengi chini ya kanisa la EAGT Mito ya Baraka, Dar es Salaam
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


Abuu Levy au waweza kumuita kwa jina la Boaz kama wengi walivyomzoea,  ni jina ambalo amelipata baada ya ubatizo. Historia yake inarejea kwenye Uislamu, ambako ndipo alilpotokea, asili yake akiwa Muarabu. Baba yake mzazi anaishi Oman hadi hivi sasa.

KWA TAARIFA YAKO licha ya kukulia kwenye famlia ya usilamu, lakini hakuwahi si tu kwenda msikitini, bali pia hata mazingira ya ndani ya msikiti hakuyafahamu yalivyo. Neema imetokana na kulelewa na mama yake mkubwa ambaye ni mlokole.

Alipotimiza umri wa miaka kumi, Abuu alikata shauri na kuokoka. Lakini KWA TAARIFA YAKO pamoja na baba yake mzazi kuwa shekhe, hakuleta kipingamizi chochote zaidi ya  kumsihi tu kuwa asimuache Mungu. Hii ni tofauti na wazazi wengine ambapo huwa vita.

Pamoja na kupewa baraka na baba yake mzazi, bado hali haikuwa nyepesi kwa baadhi ya ndugu, kwani Abuu amepitia magumu mengi, maana kila mtu alikuwa anasema lake jambo. Hata hivyo kwa KWA TAARIFA YAKO msimamo ulisalia kuwa uleule, hakukuwa na kurudi nyuma.

Abuu, mwenye umri wa miaka 24 kwa sasa ni mwimbaji wa nyimbo za injili kwa muda wa miaka nane sasa huku akiwa na album tatu hadi sasa, kati yake mbili zikiwa madukani tayari.


Mungu huandaa na kubadilisha watu wake kuanzia mmbali, maana ametujua tangia hatujazaliwa. Naye Abuu yuko kwenye mission na Mungu. Yuko katika utumishi wa Yehova.

Hiyo ndio KWA TAARIFA YAKO, vinginevyo tukutane wiki ijayo


Share on Google Plus

About John Maulid

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.