MWANACHUO MTANZANIA ASULUBIWA NA KUCHOMEWA GARI NCHINI INDIA

Mabaki ya gari alilokuwa akiendesha Mtanzania ©DailyO
Mtanzania mmoja aishie India, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kushambuliwa na kuchomewa gari yake, kisha kutembezwa uchi, kama adhabu ya kosa lililofanywa na muafrika mwenzake kutoka Sudan.

Tukio hilo ambalo limeripotiwa kutokea Jumapili tarehe 31 January, linaelezwa kushuhudiwa na polisi huku wakishindwa kuchukua hatua yoyote kwa mujibu wa mashuhuda. Hali hii inazidi kuipa India picha mbaya, taifa ambalo pia lina ripoti mbalimbali za unyanyasaji kwa wanawake.

Mlolongo wa matukio

Mitaa ya Bangalore, ajali ya gari inatokea, ambapo gari moja ilitokuwa ikiendeshwa na mwanaume kutoka Sudan, inamgonga mtu mmoja anayetajwa kuwa na umri wa miaka 35 na kufariki papo hapo. Dakika 30 baadae, mwanadada mtanzania mwenye umri wa miaka 21 akiwa na wenzake wanne wanapita eneo la tukio ambapo wanasimamishwa na kisha kuteremshwa kwenye gari yao.

Kinachofuata ni kushambuliwa miili yao, na kisha Mtanzania huyo kuvuliwa nguo zake na kisha kutembezwa hadharani akiwa mtupu. Gari yake nayo inachomwa moto. Mtu mmoja aliyejitokeza na kumpa tshirt apate kujihifadhi, naye anashambuliwa. Ni tukio la namna yake.

Kwa mujibu wa India Today, Polisi walikuwa wameshafika eneo la tukio tayari, lakini katu hawakuthubutu kuingilia kati tukio hilo la kunyanyaswa kwa watu hao, na kwamba hata walipoenda hospitali, walikataliwa huduma. Tayari ubalozi wa Tanzania nchini humo umeripotiwa kuagiza uchunguzi kufanyika kutokana na jambo hilo.

Kwa mujibu wa DailyO ya India,  tukio hilo linachochewa na ubaguzi wa rangi nchini humo, pamoja na sababu kadha wa kadha za kisiasa.

India ni taifa lenye wanafunzi wengi kutoka Afrika, Tanzania ikiwemo, ambapo mdada aliyeshambuliwa ametajwa kuwa kimasomo nchini humo, akichukua Shahada ya Usimamizi wa Biashara, BBA.

Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.