MUNISHI NA JESSICA BM KUPAMBA TAMASHA LA PASAKA

Na Mwandishi WetuWaimbaji nyota wa Nyimbo za Injili Faustin Munishi anayeshi Nairobi, Kenya na Jessica Honore ‘BM’ wamethibitisha kupamba jukwaa la tamasha la paska litakaloanza kufanyika Machi 26 Mkoa wa Geita.

Akizungumza jana Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama, alisema kuwa waimbaji hao wametihitisha kuimba siku hiyo, ambako bado kamati hiyo itaendelea kutaja waimbaji wengine wakubwa kwani bado iko kwenye mazungumzo nao.

Msama alisema kamati yake inaendelea kuchagua waimbaji watakaoimba katika mikoa wa Mwanza Machi 28, wilaya ya Kahama Machi 27 na Geita kwakuwa waimbaji ni wengi wanaomba kuimba katika tamasha hilo la kimataifa.

Msama ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Msama promotions, amesema kwa kuwa kamati hiyo kwa maka huu inatoa nafasi kubwa kwa waimbaji wa ndani amboa ndio wengi walioomba wanaangalia namna ya kukubaliana hivyo huenda kukawa na waimbaji wengi zaidi katika tamasha hili la kuliko yaliyowahi kufanyika mikoani.

Amesema Munishi ni mwimbaji wa kwanza aliethibitisha kutoka nje ya Tanzania huku akisistiza kuwa huenda wakamalizia na wengine kutoka Afrika kusini na nchi nyinginezo za Afrika.

Msama ilieleza kuwa kamati yake imeamua kumleta Munishi kutokana na maombi ya wadau mbalimbali wa muziki wa injili hapa nchini .

“Naomba niwafahamishe mashabiki wa muziki wa Injili kwamba tumekubali maoni yao, sasa wajipange kumpokea Munishi na atatumbuiza Mwanza, Kahama na Geita wakae mkao wa kupokea Neno la Mungu kupitia mtumishi wa Mungu” amesema Msama

“Kama mnavyojua mwaka huu tunatimiza miaka 16 tangu tuanze Tamasha la Pasaka, hivyo tunaleta kitu tofauti kabisa,” alisema Msama na kuongeza kuwa hivi sasa Munishi pia ni mhubiri wa neno la mungu..

Baadhi ya nyimbo zilizompa umaarufu Munishi ni pamoja na Malebo, Siasa na Injili, Paka Kulia Usiku, Kuhubiri ni Taalum, Jirani, Jirani Mchokozi, Fasheni ni Yesu, Nimeamua Mwenyewe na Maji Yana Mdudu.

Kwa mujibu wa Msama hilo litakuwa tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu na litakuwa na tofauti kubwa ukilinganisha na matamasha mengine yaliyowahi kuandaliwa na kampuni yake.

Msama alimalizia kusema licha ya kuja mwimbaji wa ndani Jesca BM ambaye anatamba na baadhi ya nyimbo kama ‘Napokea’, Nakuabudu na Nimezima Ukimya,’ waimbaji wengine waliothibitisha ni pamoja na Rose Muhando na Bonny Mwaitege.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.