NAINUA MACHO YANGU JUU KATIKA PICHA


Kuamua kuachana na ajira ili kufanya yale yaliyo moyoni sio jambo jepesi, hasa pale ambapo ajira imekuwa chanzo cha mapato kwako. Lakini hatamu hii imechukuliwa na mwanadada Furaha Isaya, ambaye ameona fika namna ambavyo anaugua moyo pale asipofanya shughuli ya uimbaji kwa kujitoa kote.

Mapema mwisho mwa mwaka jana amezindua wimbo wa 'Nainua Macho Yangu', huu wimbo umetokana na kupitia mapito kadhaa na kujihisi kuwa yuko peke yake. Pamoja na yote, akafikia kumshukuru Mungu.

Wimbo huu umetungwa mwaka 2014 na kuwepo tu kwa takriban miezi saba, ambapo pamoja na yote umedumu kwa muda wote huo kutokana na kurekebisha mambo kadha wa kadha.

Furaha sio mgeni sana wa live perfomance, na ndio maana siku 5 tu za mazoezi zilimtosha, GK imekuwepo na itakuletea video za tukio hilo akiimbia live.

Lakini pamoja na kupitia mapito yote hayo, na hata kufikia kushindwa kuamini namna ambavyo Mungu amemvusha, ndio sababu inayompelekea Furaha kutukumbusha kwamba bado Mungu yuko nasi.

Tukio mojawapo ambalo anakumbuka ni kuomba kwa malalamiko akisikitika, ndiposa akasikia sauti kwa mara ya kwanza ikimumbia kwamba mahali popote ambapo amepitia Mungu bado hajamuacha, hata mahala pale ambapo pameonekana pagumu sana.

Na hii iko miongoni mwetu sote, licha ya mapito mengi ambayo tunapitia, tutambue ya kwamba ni Mungu anatuandaa kwa jambo fulani kubwa ambalo wala hatulifahamu.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo;

The Jordan Band wakimsindikiza Furaha kuingia

Mama Mchungaji Sunga akinena jambo

Furaha na Jessica BM


Tazama picha zaidi kwa kubofya hapa https://flic.kr/s/aHskueK8JA

 Ama kupitia 'slideshow' hapa chini.
Furaha Isaya Boxing Day Party

Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.