SOMO: ILIPOSHINDIKANA ALIMTUMA MIKAELI - MCH MACHUMU

RP MAXMILIAN MACHUMU (Ufufuo na Uzima Dar es Salaam)
Mungu ana namna tofauti ya kuyafanya yale ambayo yameshindikana yatokee kwa watu wote. Hii ni habari njema kwetu.
Kwenye mambo ya kutumwa, anayetuma lazima awe na mamlaka makubwa kuliko aliyetumwa. Ukiona mtu ametumwa mojawapo ya sifa mama shati moja la aliyetumwa lazima afanye kama anavyotaka aliyemtuma, hatakama hiwezekani ni lazima amtii yule aliyemtuma.

"Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi. Sasa nimekuja kukufahamisha mambo yatakayowapata watu wako katika siku za mwisho; maana maono hayo ni ya siku nyingi bado." Daniel 10: 12

Tunaona Danieli aliomba maombi na hayakutokea kama alivyoomba na siyo kama Mungu analikana Neno lake au hakuyasikia maombi yake. Danieli aliomba kwasababu alivisoma vitabu na akagundua kwamba wayahudi waliambiwa watatoka utumwani baada ya miaka 70 na alipogundua miaka ile imekwisha ya kukaa utumwani, danieli alitubu na kufunga lakini hakuona dalili yeyote ya majibu ya maombi yake.

Danieli alimtafuta Bwana kwa bidii mpaka akampata. Lazima kuomba bila kuchoka wala kukata tamaa, Mungu amesema tumtafute kwa bidii maadam anapatikana. Unapomwomba Mungu kwa kufunga mara ya kwanza na bado hauoni jambo lolote endelea kuomba bila kuchoka mpaka kitokee kitu unachotaka.

Watu wengi wamezoea kuomba maombi ya kusihi bila kuomba maombi ya vita, Mungu hujibu mapema maombi yetu lakini majibu yanapokuwa yamekuja kwetu huwa kuna mkuu wa anga ambaye huyazuilia majibu yetu yasitokee.

Kwenye maisha yako kama wewe ni mwombaji lazima uwe na maombi ya staili mbili, msifu Mungu mwabudu, msihi kwa kutambua uwezo wake umwombe kwa kumsihi kwa unyenyekevu. Baada ya maombii ya kusihi anza kuomba maombi ya vita kwenye ulimwengu wa rohoni dhidi ya shetani na falme zake, mamlaka, wakuu wake, na majeshi ya pepo wake wote na uwakamate na mizimu ya familia na majini uwafyeke wote kwa jina la Yesu kristo.

Mikaeli alikuja pale mambo yaliposhindikana na kushughulikia wale waliozuia na danieli akapata majibu yake.

Yuda1: 9 Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.

Mikaeli ni malaika mkuu.

Ufunuo wa Yohana 12: 7 "Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu."

Danieli12: 1 "Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile."

Sehemu zote tumeona Mikaeli ni malaika mkuu wa vita. Ukiona mambo hujayapata kama inavyotakiwa maana yake yupo azuiaye mahali amejificha hivyo fanya vita vya kiroho na utafanikiwa kwajina la Yesu.

Matendo ya Mitume 13:8 "Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani"

Akina elima wapo mpaka leo, duniani wasingekuwepo wachawi maisha yangekuwa mazuri sana na Mungu anawajua sana ndiomaana ametuambia tusiwaache waishi. Mungu anaaibika kwasababu watu wake hawaishi vizuri sababu watu wake walio wengi hawajui jinsi ya kuwashughulikia shetani na mawakala wake mpaka wawaachilie. Sio kwamba mambo yameshindikana bali kuna mkono wa mtu na hujawahi kuomba maombi ambayo Mungu hayasikii.

Yupo saizi ya ibilisi ambaye anaitwa Malaika Mikaeli. shetani alikuwa malaika lakini alimwasi Mungu na Mikaeli ndiye aliyemshughulikia.

ibilisi huyu alikuwa na uwezo wa kupiga kinubi na kuweka uwepo mbinginu kwa namna ya ajabu, malaika mwingine aitwaye Gabrieli alikuwa amepakwa mafuta kwenye mambo ya kupeleka habari. Munugu alimwandaa malaika Mikaeli kwenye mambo ya ulinzi mbinguni kama jemedari mkuu na malaika mkuu, Mikaeli alipoumbwa na Mungu hakupewa uwezo wa kuimba au kupeleka habari bali alipewa uwezo wa kupigana vita.

Malaika Gabrieli aliyezuiliwa alipotua kwenye nchi, nchi ilitikisika. lakini kwa uwezo wake huu alizuiliwa na mkuu wa uwajemi, Malaika mikaeli ndiye aliyempiga mkuu wa anga aliyezuia majibu ya maombi ya Danieli.

Kwenye wokovu lazima kupigana sababu shetani mwenyewe ni mkorofi na alishawahi kupigana Mbinguni kwa Mungu Mkuu,na mikaeli ndiye aliyempiga na kumtupa nje mpaka kuzimu. Aliyempiga ibilisi miaka ile na aliyemfunga mkuu wa uwaemi miaka ile hajawahi kufa bado yupo hai. Leo tutamwambia mikaeli na majeshi yake afanye vita pamoja na sisi dhidi ya ibilisi. ukitaka upigane vita kwenye kiwango cha juu ni lazima umtumie Mikaeli.

Katika maisha kuna wtu wanaosumbuliwa na mapepo. Kuna pepo anayeitwa maimuna ambaye anafanya kazi ya kuchochea uzinzi na uasherati kwa watu hata kwa watu wa Mungu na hufanya kazi wakati wa usiku, unakuta mtu anajaribu kuacha tabia ya uzinzi lakini shetani huyu anamfanya aone sio jambo rahisi kuliacha. mwingine anaitwa maulana ambaye huleta uchafu kwa watu na uvivu wa kuoga. anafanya watu wawe wachafu. mwingine anaita jahasa ambaye kazi yake ni ulevi wa pombe, sigara, bangi na huyu jahasa ndiye huwafanya watu wasiache mambo hayo. Rohani ni shetani anayeleta uvivu, usingizi kwenye maombi na kusoma neno la Mungu na kwenye ibada, kwenye kufanya kazi za Mungu mtu anakuwa mvivu kupitiliza lakini kwenye mambo mengine ambayo siyo ya kimungu anakuwa kawaida. Mwingine anaitwa makata ambaye huleta magonjwa ambayo mtu akiombewa anashindwa kupona, huyu ni shetani wa mauti ambaye analeta magonjwa yaliyoshindikana, unafunga na kuomba na kuombewa sana lakini shetani huyu anakuwa mgumu kukuachia lakini Yupo Jemedari kiongozi wa vita Mikaeli ndiye tutamtumia kwenye vita dhidi ya mashetani haya, kuna fausta ambaye huleta umaskini, fukra huyu ni shetani anayewazuia watu wasitoe fungu la kumi, shetani mwingine abasa huleta hasira, wivu na ujeuri. shetani mwingine silikavu ambaye huleta umaskini kwa watu na kuwafanya wawe ombaomba

Ukiona mambo kwenye maisha yako yameshindikana usifikiri Mungu hajakusikia maombi yako na amekuacha, kuna kizuizi cha mkuu wa anga mahali ambaye amekuzuia na huyo lazima ashughulikiwe na yale majibu yako yaje kwako kwa jina la Yesu.

Yupo malaika Mikaeli mkuu wa majeshi ya malaika ambaye tutamtumia ili tupigane na huyu mkuu wa anga na wakala zake waliozuia baraka zetu kwa jina la Yesu. mashetani wote waliojificha kwenye ulimwengu wa rohoni lazima tuwafuate na kuwateketeza kwa jina la Yesu.

Malaika mikaeli ni kiumbe wa Rohoni na wale waliokuzuia nao ni viumbe wa Rohoni na hakuna jambo gumu la kumshinda Mungu wetu. Mikaeli anajua mbinu za vita na leo tunaungana na majeshi ya malaika Mikaeli ili kupigana na mkuu wa anga la uajemi na mapepo yake.

Ukiri:
Katika jina la Yesu kristo ninaagiza malaika Mikaeli na majeshi yako kuwakamata wote walionizuia kwenye maisha yangu, walionizuia kwenye ndoa, kazi, huduma, safari, biashara, Elimu ninaamuru wakamate wote na kuwateketeza kwa damu ya Yesu kristo, ninawafyeka mawakala wote wa shetani walionizuia nisifanikiwe kwa jina la Yesu, ninawateketeza kwa jina la Yesu.

Binti huyu anafanya kazi kwenye hoteli maeneo ya mwananyamala na huwa anatoka usiku saa saba, katikati ya wiki wakati anatoka kazini alikutana na mtu mweupe mrefu sana akamnyooshea mkono na kumwambia asimwambie mtu na wakati alipofika nyumbani alimwelezea jirani yake kilichompata na mara akaanza kushindwa kula na kupoteza ufahamu kuwa kama mtu mwenye matatizo ya akili, ndugu yake alielezea kwamba alimpeleka hospitali ya mwananyamala wakamwelekeza aende muhimbili na walipompeleka wakawaandikia kwamba tatizo lake haliwezekekani kutibiwa pale na ndipo waliporudi nyumbani na kwa bahati nzuri jirani yao ambaye anasali Ufufuo na Uzima akawaeleza wampeleke kanisani.

Akiwa anatokwa na mapovu mdomoni na kukonda sana kwa kutokula kwa siku nne wakati wa maombi alifunguliwa na kupona udhaifu uliokuwa unamsumbua na akaweza kula chakula ambacho mwanzoni alishindwa kula sababu kilikuwa hakipiti kwenye koo. Bwana Yesu amemwokoa kutoka kwenye mauti na kumweka huru, yeye na ndugu zake wamempa Bwana Yesu maisha yao na kuahidi kumtumikia siku zote za maisha yao.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.