SOMO: VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU - MWAL MWAKASEGESEMINA YA NENO LA MUNGU..
VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU.
NA MWL MWAKASEGE
ARUSHA MJINI UWANJA WA RELI

Kusoma sehemu iliyopita BONYEZA HAPA
                                                   


Marko 11: 27-28 ‘’ 27Wakafika tena Yerusalemu, wakati Yesu akitembea hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia.

28Wakamwuliza, “UNAFANYA MAMBO HAYA KWA MAMLAKA GANI? Naye ni nani aliyekupa MAMLAKA YA KUFANYA HAYO?

Kuna kiwango cha maisha ambacho huwezi kufikia kama hujajua kutembea ndani ya mamlaka uliyopewa na Yesu.Jana tuliangalia mamlaka ambazo Mungu kazitoa kwa ajili yetu.Mwanza 1:28 neno akawabarikia maana yake ni akawapa vitu ndani mwao ili wawe na uwezo wa kufikia kiwango ambacho Mungu anataka wafikie.

Ndio maana aliwapa Baraka ya kuwa zaeni. Lakini kuna baadhi ya nchi wameweka sheria kuwa wasizae mtoto zaidi ya mmoja ina maana Mungu ameondoa Baraka zake katika uzazi.Baraka maana yake ni kukuwezesha kufikia viwango ambavyo Mungu anataka uwe navyo.

2 POINTI YA 2: KUJUA KUWA MAMLAKA NA MATUMIZI YAKE NI JAMBO LA KISHERIA 2..

Na sheria yenyewe ipo kwenye ulimwengu wa roho. Na hapa tunaona mamlaka ya kutawala wamepewa Adamu katika sura ya kwanza ya kitabu cha mwanzo muda huo ambapo walikuwa ni roho tu. Kwa hiyo hili jambo la sheria ni jambo la kiroho kwanza kabla halijawa la kimwili.

*SHERIA NA MAMLAKA VINAFANYA KAZI KWA KUSHIRIKIANA

Mimi nimesoma sheria ya biblia japo sheria ya kawaida sijasoma ila ya kwenye biblia ndio nimeisoma vizuri sana. Sheria imetoka kwenye biblia japo kuna mambo ambayo yanaingilia na hii sheria ya kawaida. Na jua hili suala la kuwa hakuna mamlaka bila sheria na hakuna sheria bila mamlaka. Na sheria bila mamlaka haina nguvu na mamlaka bila sheria haina nguvu. Ukitaka kubadilisha sheria lazima kwanza ubadillishe mamlaka na ukitaka kubadilisha mamlaka badilisha sheria.

πŸ“–

Daniel 7:25 ‘’25Atanena maneno kinyume cha Aliye Juu Sana na kuwaonea watakatifu wake Yeye Aliye Juu Sana, huku akijaribu kubadili majira pamoja na sheria. Watakatifu watatiwa chini ya mamlaka yake kwa wakati, nyakati mbili na nusu wakati’’.

Kwa hiyo ukiangalia mistari hiyo utaona kuwa ili kuweza kuwabana watakatifu iliwapasa kubadili majira na sheria kwa lengo la kudhoofisha na kuua nguvu za watakatifu.

Hili neno kwa Nyakati mbili na nusu ina maana kuwa ni kipindi Fulani ambacho kuna kitu wanataka kupitisha kwa ajili kuwafunga watakatifu. Na kuwafanya wawe dhaifu kwenye majira na sheria. Ukitaka kuwadhoofisha watu badilisha majira na sheria.

Ukiamua kusimamia sheria ya Bwana shetani atawinda ili aweze kukudhoofisha ili ushindwe kushughulika na sheria ambazo Mungu amekupa.

SHERIA. Ni utaratibu unaotengeneza mfumo wa mwelekeo wa maisha chini ya mamlaka husika iwe ni nchi au taifa. Lakini kwa wakati wa sasa kuna sheria za kimataifa na pia kuna mahakama ya kimataifa ili iweze kusimamia sheria.

Kumbuka hili siku zote kuwa sheria bila mamlaka inakuwa haina nguvu na ili mamlaka iwe na nguvu lazima iwepo sheria ya kusimamia na ili sheria iwe na nguvu lazima iwepo mamlaka ya kusimamia sheria. Kwa mfano chombo cha kusimamia sheria ni mahakama. Kwa hiyo mahakama bila sheria haina mamlaka na mahakama haina nguvu pasipo sheria. Tuko pamoja mpaka hapo?

Nakumbuka kuna mtu mmoja alisema biblia ni kitabu cha sheria, au unaweza sema biblia ni kitabu cha kuongoza utaratibu wa maisha ya mwanadamu kama Mungu anavyotaka.

☀MFUMO UNAONGOZA SHERIA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NI MAMLAKA YA KIUTAWALA NI YA KIFALME.

Kwa hiyo ukitaka kuimarisha mamlaka lazima utafute sheria zinazosimamia hiyo mamlaka.

Daniel 2:27-45. Hapa tunaona habari za Nebukadreza na ndoto yake. Na kuanzia mstari wa 27-30 tunaona Daniel akitoa maana ya ndoto ya mfalme Nebukadreza na ilikuwa ni hakika Mungu ataithibitisha ile ndoto.

Katika hali ya kawaida ambayo Mungua aliumba ulimwengu uliumbwa ili uendeshwe kwa mfumo wa Kifalme na sio Kidemokrasia. Japo kuna sheria za mifumo yote hii miwili ila Mungu aliumba ulimwengu kwa mfumo wa kifalme.

Waefeso 6:12 Kwa maana kushindana kwetu si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho. Kwa hiyo tunaona katika ulimwengu war oho tunapambana na falme maana hakuna demokrasia kule.

Daniel 7:21-22, 25-27.’’

21Nilipoendelea kutazama, pembe hii ilikuwa inapigana vita dhidi ya watakatifu na kuwashinda, 22mpaka huyo MZEE WA SIKU (YESU) alipokuja na kutamka hukumu kwa kuwapa ushindi watakatifu wa Yeye Aliye Juu Sana, na wakati ukawadia walipomiliki ufalme.

’25Atanena maneno kinyume cha Aliye Juu Sana na kuwaonea watakatifu wake Yeye Aliye Juu Sana, huku akijaribu kubadili majira pamoja na sheria. Watakatifu watatiwa chini ya mamlaka yake kwa wakati, nyakati mbili na nusu wakati’’. 26‘ “Lakini ndipo mahakama itakapokaa kuhukumu, nayo mamlaka yake yataondolewa na kuangamizwa kabisa milele. 27Ndipo ufalme, mamlaka na ukuu wa falme chini ya mbingu yote utakabidhiwa kwa watakatifu, watu wa Yeye Aliye Juu Sana. Ufalme wake utakuwa ufalme wa milele, nao watawala wote watamwabudu na kumtii Yeye.’

Umeona hapo , Shetani akivuruga majira anavuruga na sheria na mwisho anavuruga na hukumu.Lakini hukumu itawekwa nao watamwondolea shetani mamlaka katika ulimwengu wa roho.

Kwa jinsi Mungu alivyomuweka alikuwa Bwana Jela kwa wana wa Israel ndio maana kiti chake kilikuwa na pingu na alitakiwa kuwafunga wana wa Israel hadi Muda utakapowadia. Ndio maana Nebukadreza alipokiuka maadili ya kazi yake ambayo Mungu alimpa ilibidi aondolewe kwenye nafasi yake Mungu alimwambia hukumu hii imekuja kwa kwa amri ya walinzi ambao ndio walikuwa waombaji. Na alisema atarudishwa mpaka atakapokumbuka kuwa mbingu ndio zinazotawala. Lakini mtoa amri ni mlinzi yaani mwamboji ndio maana Yesu alisema nimeweka walinzi juu ya kuta zako ee Yerusalemu ambao hawatanyamaza mchana wala usiku.

☀SHERIA NA MAJIRA VINA UWEZO WA KUIMARISHA NA KUDHOOFISHA MAMLAKA.

Mungu aliweka nyakati na ndipo akamuweka mwanadamu ili aweze kuishi kwa kadri nyakati zile zilivyowekwa.

πŸ‘‰πŸΌNdio maana mtu aakikuibia muda anakuwa kakuibia muda maisha, na mtu akikupotezea muda ina maana anakupotezea muda.

Majira na nyakati zinaenda pamoja na ndio maana utasikia huku mjini watu wakisema sheria imepitwa na wakati kwa hiyo inapaswa kuwa kila majira yakibadilika nayo sheria inapaswa ibadilike ili kuweza kuendana na wakati uliopo. Biblia peke yake ndio sheria zake hazibadiliki kabisa.

πŸ‘‰πŸΌPOINT 3: UIMARA WA MAMLAKA YAKO HAOA DUNIANI INATEGEMEA UNAAMINI NA UNAJUA KWA KIWANGO GANI KUWA MBINGU NDIZO ZINAZOTAWALA.

Daniel 7:26-27 na Daniel 4:26 ‘’ naye humtawaza ye yote amtakaye. 26Amri ya kuacha kisiki pamoja na mizizi yake inamaanisha kwamba ufalme wako utarejezwa kwako utakapokubali kwambaπŸ‘‰πŸΌ MBINGU NDIZO ZITAWALAZO.’’ Na Kumbuka kuwa MBINGU NI KITI CHA ENZI CHA MUNGU.

Ayubu 38:33 ‘’ 33Je, unajua sheria zinazotawala mbingu? Waweza kuweka utawala wa Mungu duniani?.

Kwa hiyo ili umjue Mungu vizuri zijue sheria zake.

Ukitaka kuijua biashara vizuri zijue sheria za biashara vizuri.

Ukitaka kilimo vizuri jua sheria za kilimo. Kwa mfano kuna baadhi ya mazao yamewekewa sheria hata kama kama ni ya kwako hairuhusiwi kung’oa. Mfano chai uking’oa chai hata kama ni ya kwako hairuhusiwi. Na uking’oa unashtakiwa kwa mujibu wa sheria.


πŸ‘‰πŸΌPOINT 4: UWEZO WA MUNGU NA MAMLAKA YA MUNGU INATAKIWA IFANYE KAZI KWA SHERIA YA NENO LA MUNGU.

Luka 9:1-2 ‘’Yesu akiisha kuwaita wale kumi na wawili pamoja, aliwapa MAMALAKA NA UWEZO wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote, 2kisha akawatuma waende wakahubiri UFALME WA MUNGU na kuponya wagonjwa’’

Kwa hiyo ina maana ukipewa uwezo na mamlaka na ufalme wa Mungu unakuwa tayari upo. Kwa sababu hakuna mamlaka isiyokuwa chini ya Mungu.
πŸ“–Mathayo 12:28-29 ‘’ 28Lakini kama Mimi ninatoa pepo wachafu kwa Roho wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umekuja juu yenu.

29“Au tena, mtu awezaje kuingia katika nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali zake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Akiisha mfunga, ndipo hakika anaweza kuteka nyara mali zake.


πŸ‘‡πŸ‘‡

Umeelewa hapo Yesu alipokuwa na mamlaka ya kutoa pepo na alipokuwa anatoa pepo ina maana alikuwa naleta na ufalame wa Mungu. Na ndio maana alisema ‘’ mtu awezaje kuingia katika nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali zake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Akiisha mfunga, ndipo hakika anaweza kuteka nyara mali zake’. Kwa hiyo ujio wa Yesu ulikuwa chini ya sheria ambayo ilisimamiwa na mamlaka ya mbinguni.

πŸ‘‡

Kumbuka kuwa mamlaka ni uwezo wa kisheria wa kuta amri na kusimamia kile ilicho amuru. Kwa mfano niliulize swali je mkuu wa wilaya anaweza mfukuza kazi mkuu wa mkoa?

πŸ‘‰πŸΌ ’ukweli ni kuwa anaweza fanya hivyo ila hana uwezo huo na mamlaka ya kusimamia utekelezaji wake mpaka mamlaka nyingine ambayo ndiyo inaweza kuwa na nguvu za kumfukuza kazi.

Pia angalia mfano wa wana wa skewa katika
πŸ“– Matendo Ya Mitume 19:11-17.

Wana wa skewa walikuwa wapunga pepo na walijua kuwa Paulo alikuwa nauwezo juu yao nao wakasema isiwe tabu nao wafanye kama Paulo. Na wakamwambia yule mtu mwenye pepo kwa jina la Yesu anayehubiriwa na Paulo mtoke huyu. Yule pepo alisema kuwa Paulo namfahamu na Yesu namfahamu nyie ni nani? Hili lilikuwa ni swali lakisheria.

πŸ‘‡πŸ‘‡

Fahamu sana hii siri itakusaidia. Kwa mfano Raisi popote alipo analindwa sana , usisikie tu Obama yuko mtaani au dukani kununua vitu kama wegine hapo ujue hayuko peke yake alia na walinzi wengi hata kama huwaoni. Pia ulinzi wa Mtu unategema sana nafasi aliyonayo huyo mtu.

πŸ‘‡πŸ‘‡

Soma Isaya 49:24,’’ 24Je, nyara zaweza kuchukuliwa kutoka kwa mashujaa wa vita, au mateka kuokolewa kutoka kwa watu wakali?.. Je aliye hodari aweza kuokolewa na mateka yake.

πŸ“–

Matendo 10 :38 ‘’ 38Jinsi Mungu alivyomtia Yesu wa Nazareti mafuta katika Roho Mtakatifu na jinsi Shetani, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye.

Kwa hiyo lazima ucheki katika kuwa ni sheria ipi ambayo inaweza kuwafungua wafungwa halali? Ndio maana kasema mateka yake maana si wote waliofungwa kuwa wameonewa na shetani.


☀KUWAFUNGUA WATU WALIOMILIKIWA NA FALME MBILI KWA WAKATI MMOJA.

Wakorintho 5: 4-5 4Mnapokutana katika Jina la Bwana wetu Yesu nami nikiwepo pamoja nanyi katika roho na uweza wa Bwana Yesu ukiwepo, 5mkabidhini mtu huyu kwa Shetani, ili asili ya dhambi iangamizwe lakini roho yake iokolewe katika siku ya Bwana,’’

πŸ‘‡πŸ‘‡

Mtu huyu alikabidhiwa kwa Shetani mwili wake na roho yake ikakbidhiwa na Yesu na Yesu alikuwepo je mtu huyu unamfunguaje sasa.

Kwa hiyo ili kumsaidia mtu huyu inakupasa ujue mamlaka na sheria ili ujue cha kufanya.


πŸ™‡πŸΌKAZI YA SHERIA.

Sheria zote zilshatungwa na Mungu. Na katika ulimwengu wa Roho kuna sheria kuu mbili tu.

πŸ‘‡πŸ‘‡

1: SHERIA YA UZIMA.

2: SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI.

Shetani hawajawahi kutunga sheria yoyote na wala hata ufalme wake ni wa kucopy.na anachofanya shetani anajua kuitumia sheria ya dhambi na mauti.

πŸ‘‡

Na sasa ili kumshinda inahitaji maarifa maana biblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa na sio kwamba shetani yupo. Ndio maana Yesu leo kakuletea maarifa haya ili ujue namna na kumshida shetani.

πŸ“–

Wagalatia 3:24.24Hivyo, sheria ilikuwa kiongozi kutufikisha kwa Kristo, ili tupate tuhesabiwa haki kwa Imani.

Kazi kuu ya sheria ni kutuleta kwa KristoChunguza sheria zilizoko huko uliko au ni kazini au kanisani au mahali popote. Je inakuleta kwa kristo au inakupeka mbali na Mungu. Ndio maana biblia inasema pasipo maono watu huacha kuziuia ila anaheri mtu yule anayetii sheria.

Ukitaka kuona nchi inataka ikupeleke wapi cheki sheria/katiba ya nchi hiyo.
Itaendelea kesho
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.