SOMO: VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU - MWAL MWAKASEGE

SEMINA YA NENO LA MUNGU (day 4)
VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU.
NA MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE
ARUSHA MJINI UWANJA WA RELI

kusoma sehemu ya tatu iliyopita Bonyeza Hapa

Marko 11: 27-28 ‘’ 27Wakafika tena Yerusalemu, wakati Yesu akitembea hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia.

28Wakamwuliza, “UNAFANYA MAMBO HAYA KWA MAMLAKA GANI? Naye ni nani aliyekupa MAMLAKA YA KUFANYA HAYO?

Siku ya kwanza tuliangalia mamlaka 11 ambazo Yesu katupa kama watu wake.Katika kitabu cha Mwanzo 1:28 Mungu akawabarikia akasema zaeni mkaongezeke na mkaijaze nchi na kuitisha.Baraka ya Mungu ni vitu/mawazo ambayo yatakuwezesha kufanikiwa.

SUMMARY YA POINT YA 3: KAZI ZA SHERIA KWA SURA YA BIBLIA:

i):Kutengeneza mfumo na mwelekeo wa maisha.

Mithali 29:18 Kazi ya sheria ni kulinda maono yaliyoko.

ii): Kutuongoza na kutuleta kwa Kristo.

Wagalatia 3:24 Tangu bustani ya Edeni sheria zilikuweko ili kuweza kumwongoza mwanadamu

iii):Kujua kipi ni halali na kipi si halali.

‘’neno halali halitumiki sana kwenye biblia bali hutumika neno kibali. Kesho tutaangalia uhusiano wa sheria na neema ya kristo.

iv): Kusimamia haki na hukumu kwenye nafasi ya mamlaka.

Zaburi 97:1-2 ‘’ BWANA anatawala, nchi na ifurahi, 2 visiwa vyote vishangilie. Mawingu na giza nene vinamzunguka, haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake cha enzi

v): Kutengeneza aina ya maisha.

Kuna tofauti ya aina ya maisha na mfumo wa maisha. kwa mfano kuna tofauti ya mfumo wa engine ya Toyota na aina ya gari la Toyota. Kwa hiyo Jua kutofautisha kati ya mfumo wa maisha na aina ya maisha.Warumi 8:2 ‘’ 2 Kwa sababu SHERIA YA ROHO WA UZIMA katika Kristo Yesu imeniweka huru mbali na SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI

Hapa tunaona aina mbili ya Sheria sheria ya Roho wa uzima na Sheria ya dhambi na mauti.

Biblia inaposema dhambi iliingia ulimwenguni, ina maana kuna mahali dhambi ilikuwepo na ilipofunguliwa mlango ndio ikaingia ulimwenguni. Na Mauti ikatawala kuanzia Adamu hadi Musa, na hapo ndipo Mungu alipoanza kuachilia katika ulimwengu wa roho sheria na katika ulimwengu wa mwili ili zipate kumsaidia mwanadamu.

Yohana 10:10 ‘’ 10Mwivi huja ili aibe, kuua na kuangamiza. Mimi nimekuja ili wapate uzima kisha wawe nao tele’’ Kwa hiyo Yesu alikuja na aina ya maisha na mfumo wa maisha ambao ni wa ngazi ya juu sana tofauti na ule wa agano la kale.

SABABU YA 5: KUJUA SEHEMU YA MWILI WA MWANADAMU KATIKA ULIMWENGU WA ROHO KUTAWALA ULIMWENGU WA MWILI.

Zaburi 8:3-8’’ Zaburi inaelezea jinsi Mungu alivyomtawaza mwanadamu juu ya vitu. Angalia Zaburi 115: 16 ‘’ 16Mbingu zilizo juu sana ni mali ya BWANA, lakini dunia amempa mwanadamu. Hapa tunaona kabisa ya kuwa Mungu kamtawaza mwanadamu ili awe ndio mmiliki wa dunia.Point ya Muhimu sana hapa ni kujua sehemu ya mwili wa Mwanadamu katika kutawala ulimwengu wa Roho.

Swali nililokuwa najiuliza ni kwa nini mwanadamu alipewa mwili, je kulikuwa na ulazima gani wa mwadamu kuwa na mwili. Kwa sababu ukisoma kitabu cha mwanzo sura ya kwanza utaona mwanadamu akiwa roho akipewa Baraka lakini katika sura ya pili ndipo tunaona sasa wanapewa mwili na hapo ndipo wanapewa na sheria juu ya kuishi katika bustani ya Edeni. Kwa hiyo ukitaka kuelewa sheria zilizo wekwa soma Ayubu 38

1Wakorintho 15:40 40Pia kuna MIILI YA MBINGUNI na MIILI YA DUNIANI, lakini uzuri wa ile miili ya mbinguni ni wa aina moja na uzuri wa ile miili ya duniani ni wa aina nyingine

Hapa unaona kuna mwili wa Mbinguni na mwili wa duniani. Sasa swali langu hapa ni kuwa kwanini kama hapa duniani ni mwendelezo wa ufalme wa mbinguni kwanini tusingetumia mwili wa mbinguni, kwani mwili wa duniani una kazi gani? Hili swali nilijiuliza sana ili kupata kuelewa kwa kina haya mambo.

Katika kujaribu kufafanua Zaidi nikatengeneza sentensi ifuatayo.

ROHO YOYOTE KATIKA ULIMWENGU WA ROHO IKITAKA KUTAWALA ULIMWENGU WA MWILI LAZIMA ITUMIE SHERIA ZILIZOKO KATIKA ULIMWENGU WA MWILI.

Swali utajiuliza kuwa niliipata wapi hii ntakuambia kuwa nillipata nilipokuwa najiuliza swali nilipokuwa nataka kujua uhusiano uliokuwepo kati ya mwili wa Yesu na mwili wake alipokuwa Duniani. Yaani kwanini alihitaji mwili, maana Yesu ndio aliyeziumba mbingu na nchi naye ni Mungu na muda mwingine aiingia katika bustani ya Edeni wakati wa jua kupunga na biblia haituambii kuwa alikuwa na mwili au vyovyote.

Swali hapa najiuliza ni kwanini Yesu alihitaji mwili (na mwili tayari ulikuwa na dhambi) wa hapa Duniani. Jibu NI KUWA ILI AWEZE KUIHUKUMU DHAMBI KATIKA MWILI.

1Wakorintho 15:45,47 45Kwa hiyo imeandikwa, “Mtu wa kwanza Adamu alifanyika kiumbe hai,” Adamu wa mwisho, Yeye ni roho iletayo uzima. 47Mtu wa kwanza aliumbwa kwa mavumbi ya ardhini, mtu wa pili alitoka mbinguni.

Yesu alileta uzima na ili kuweza kuleta uzima ilibidi kwanza mauti ihukumiwe maana mahakama ya mbinguni ilishapitisha kuwa mshahara wa dhambi ni mauti. Kwa hiyo ili uje uzima ilitakiwa kwanza mauti ihukumiwe.

TUANGALIE AINA ZA ROHO.

1: Mungu ni Roho.

2: Roho ya mwandamu.(Mwanadamu ni bora kuliko malaika)

3: Malaika (Wapo wale walioasi na wale watiifu)

Roho hizi zote zikitaka kutawala ulimwengu wa mwili lazima zibebe mwili. Ndio maana hata Mungu alipotaka kuja duniani upitia Yesu ilibidi aje katika mwili hivyo hivyo na shetani nae akitaka kuingia duniani lazima tu aingie katika mwili si ndio maana tunaona mapepo yanakaa katika mwili.

Warumi 8:3 ‘’ 3Kwa maana kile ambacho sheria haikuwa na uwezo wa kufanya, kwa vile ilivyokuwa dhaifu katika mwili, Mungu kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe kwa mfano wa mwanadamu mwenye mwili ulio wa dhambi na kwa ajili ya dhambi, YEYE ALIIHUKUMU DHAMBI KATIKA MWILI.

Wafilipi 2:8 ‘’ 8Naye akiwa na UMBO LA MWANADAMU, alijinyenyekeza HATA MAUTI, naam, mauti ya msalaba!

Biblia inaposema mshahara wa dhambi ni mauti ina maana ilipopatikana mauti ya mwanadamu ilikuwa sasa ndio tayari mauti imehukumiwa na dhambi ilihukumiwa katika mwili. Kwa maana hapo Yesu aliposema katika Yohana 10:10 kuwa wawe na uzima kisha nao tele alikuwa ana maanisha kuwa kupitia yeye mauti itahukumiwa na yeye ataleta uzima. Maana uzima hauwezi kuja ikiwa mwili bado utatawaliwa na sheria ya dhambi na mauti. Kwa hiyo baada ya hukumu ndipo roho ya uzima inafanya kazi. Tuko pamoja mpaka hapo?

Yohana 1;1-14 tunaona habari za neno na neno kuja kufanyika mwili nasi tukaouona utukufu wake nae neno akakaa kwetu. Waebrania 10:5 ‘’ 5Kwa hiyo, Kristo alipokuja duniani alisema, “Dhabihu na sadaka hukuzitaka, BALI MWILI ULINIANDALIA. Mungu alimwandalia Yesu mwili alipokuw hapa duniani si kwa ajili yake bali kwa ajili ya kazi ile Mungu aliyompa.

Wafilipi 1:21-24 ‘’ 21Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida. 22Kama nitaendelea kuishi KATIKA MWILI, HII NI KWA AJILI YA MATUNDA YA KAZI. Lakini sijui nichague lipi? Mimi sijui!

Paulo anasema kuishi katika mwili ni kwa ajili ya matunda ya kazi. Kwa hiyo elewa sasa kuwa Yesu ndiye kaumba kila kitu alikuwa haihitaji mwili, ile kuchukua mwili ilikuwa ni kwa ajili ya kazi maalumu ambayo Mungu alimpa. Ili tulioko duniani tuweze kufaidi matunda ya hii kazi ambayo Mungu aliyotupa ili tupate kuishi hapa duniani.

Waebrania 10:5-7,9-10 5Kwa hiyo, Kristo alipokuja duniani alisema, “Dhabihu na sadaka hukuzitaka, bali MWILI ULINIANDALIA. 7Ndipo niliposema, ‘Tazama niko hapa, kama nilivyoandikiwa katika kitabu, Nimekuja kufanya mapenzi Yako, Ee Mungu.’ Kisha akasema “TAZAMA NIKO HAPA, NIMEKUJA KUYAFANYA MAPENZI YAKO.” Aondoa lile agano la kwanza ili kuimarisha la pili. 10Katika mapenzi hayo sisi tumetakaswa na kufanywa watakatifu kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara moja tu.

Yesu kupewa mwili ilikuwa ni kwa ajili ya kuyafanya mapenzi ya Mungu.Katika Yesu kuyafanya mapenzi ya Mungu tunapewa utakaso ambao Yesu nae alipewa ili nasi tupate utakaso.

Kwa sababu dhambi ilipoingia ilishambulia mwili kwanza na roho ya mwili nayo ikangiliwa na dhambi yaani dambi iliiua roho na ikavuruga nafsi ya mtu.

Dhambi ni uasi yaani kwenda kinyume cha mapenzi ya Mungu. Ndio maana ili uweze kuitafsri vizuri dhambi inabidi uende kisheria. Watu wengi waliokoka hawajui vizuri namna ya kuitafsiri dhambi kisheria huwa wanatumia tafsiri za kawadia kawaida na bila kwenda ndani na shetani kawabana ili wasijue vizuri hata kujua maana ya dhambi.

Ni mwili wa kibinadamu ambao unaweza kubeba damu ambayo inaweza kulipa damu ambayo ndio inafuta dhambi.

UJIO WA YESU KATIKA MWILI ULIKUWA NA MAMBO YAFUATAYO

1: KULETA HESHIMA MPYA KWA MWANADAMU

Yaani ile heshima iliyokuwa imepotea. Ndani ya damu ya Yesu unapewa heshima ile ambayo Yesu alipewa yaani kuketi pamoja nae.

2: KUREJESHEWA MAHUSIANO KATIKA YA MUNGU NA MWANADAMU.

Uhai uko ndani ya damu ndio maana Mungu alikataza kula damu pamoja na nyama. Kwa sababu damu inatumika kuleta upatanisho kati ya Mungu na mwandamu. Ndio maana shetani nae akaanza kucopy na waganga nao wakawa wanahitaji kafara za wanyama ili watumie nao kuita mapepo yao. Ila Mungu alipomtoa Yesu nae shetani akataka kuiga lakini akashindwa na akishia tu kuzini na watu lakini ameshindwa kupata kama Yesu na anaishia tu kuwatoa kafara.

Yakobo 4:7-8 ‘’ 7Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. 8Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, ninyi wenye dhambi na kuisafisha mioyo yenu, ninyi wenye nia mbili.

Biblia inaposema mtiini Mungu kwanza ndipo mumpinge shetani. Shetani hamwogopi mtu ambaye hana Yesu ndani. Huwezi kumpinga shetani kama hauna nguvu za Mungu ndani yako ndio maana Yesu alisema pasipo mimi ninyi hamuwezi lolote.

Waebrania 10:6 19Kwa hiyo, ndugu zangu, kwa kuwa tunao ujasiri wa kupaingia Patakatifu pa Patakatifu kwa damu ya Yesu.

Damu ya Yesu imetuwesha kumkaribia Mungu ili aweze kutukaribia na sisi.

Waebrania 10:16 ‘’ 6“Hili ndilo agano nitakalofanya nao baada ya siku hizo, asema Bwana. NITAZIWEKA SHERIA ZANGU MIOYONI MWAO, NA KUZIANDIKA KATIKA NIA ZAO.”

Mungu anasema atiweka sheria zake katika moyo wetu. Hivyo tujitahidi sana kujua sheria ambazo Mungu.

3: MUNGU KUTURUDISHIA MAMLAKA ILIYOPO KWENYE MWILI.

Warumi 9:5 ‘’ 5Wao ni wa uzao wa mababa wakuu wa kwanza, ambao kutoka kwao Kristo alikuja kwa jinsi ya mwili kama mwanadamu,Yeye ambaye ni Mungu aliye juu ya vyote, mwenye kuhimidiwa milele! Amen

Wafilipi 2:5-10 ‘’Alijifanya kuwa hana utukufu iliapate kufanya yale mapenzi ya Mungu na watu warudishiwe kile kilichopotea.’’

Mwanzo 1:1-2 ‘’Biblia inasema hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi na baada ya hapo biblia inanyamaza. Na tunaona sura ya pili kuwa nayo nchi ilikuwa utupu na ukiwa. Ina maana hasi nchi inakuwa utupu ina maana kuna kitu kilichoondolewa ni giza. Hauoni mahali popote Mungu akiumba giza au akisema kuwe giza bali yeye alisema iwe Nuru.

Kwa hiyo tokea Mwanzo Mungu alitupa kutembea katika mwili tukiwa na mamlaka. Ndio maana utaona katika agano la kale akina Haruni ,Musa na Joshua walikuwa na miaka 80-90 lakini walikuwa na nguvu sana. Si Zaidi sana sasa ndani ya agano jipya, ukizijua siri hizi utaona tu umri unakwenda na hauzeeki.

Kwa hiyo Mungu akatupa jina lipitalo kila jina ili kwa jina la Yesu.

1.Kila GOTI lipigwe goti ni kuonesha unyenyekevu kwa Mungu. Iko siri kujua matumizi ya magoti yako kwa Mugu.

2: Kila ULIMI ukiri, ulimi ndio umebeba uzima na mauti. Na shetani anavuruga ulimi ili ushindwe kwenda sawa sawa na Mungu.

3:Kila mtakapokanyaga NYAYO zenu nimwapata kumiliki, Nyayo ni kukupa umiliki ili kila ukikanyaga uone/ waone utisho wako.

4: VIUNGO VYA UZAZI. Ni kiwanda cha kutungeneza miili, ndio maana shetani anawinda sana achezee viungo vyako vya uzazi ili kuharibu mpango wa Mungu wa namna ya kuwaleta watu duniani. Ndio maana uzao wa watu waliokoka unakuwa ni shida sana maana setani anataka kuwavuruga. Sasa sisemi uzae haraka haraka ndipo uokoke hapana. Nataka uelewe hapa jinsi ilivyo muhimu sana kulinda sana viungo vyako vya uzazi ii usije ukawatoa akina Ishamel.

Katika biblia wametumia neno VIUNO kwa mwanaume ila kwa Mwanamke wametumia TUMBO. Ndio maana Mungu alimwambia Yeremia nilikujua tokea tumboni mwa mama Yako. Paulo anasema Mungu alinitenga tangu tumboni mwa mama Yangu. Yohana alijazwa nguvu za Mungu tangu tumboni mwa mama yake. Na pia mahali pengine biblia inasema walijifunza uongo tangu tumboni mwa mama yao.

5:MIKONO YAKO, Ndio maana Mungu alimwambia Musa iniue mikono, katika baadhi ya makabila huwa hawaruhusu mtu umnyoshee kidole mtu mwingine ukiwa na hasira maana wanajua kuna kitu kinaachiliwa kwenye ulimwengu waroho.

6; MIGUU ni mizuri kama nini miguu yao waletao habari njema. Kwa hiyo kuna siri kubwa sana katika miguu.

Ukijua mamlaka hizi zilizoko ndani ya mwili wako utajua namna ya kutembea na na kuepuka dhambi. Watu wengi hawajui haya ndio maana utaona watu wameokoka vizuri ila uzinzi unawasumbua au uongo au kuvuta sigara. Wanajitahidi sana kujinanusua ila hawawezi kwa sababu hawana maarifa ndani.

Usikose sehemu ya mwisho iliyofundishwa siku ya mwisho wa semina, endelea kusoma GK
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.