VIINGILIO TAMASHA LA PASAKA NI ELFU 2 KWA ELFU 5

Na Mwandishi Wetu

Sehemu ya wakazi wa Jiji la Mwanza kwenye Tamasha la Pasaka 2014 (bofya hapa kuona)
Kampuni ya Msama Promotions imetangaza viingilio vya Tamasha la Pasaka mwaka huu kuwa ni shilingi 5000 kwa wakubwa na shilingi 2000 kwa watoto.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi, Alex Msama alisema viingilio hivyo vinaendana na tukio hilo ambalo mbali ya kumuimbia na kumtukuza Mungu pia lina dhamira ya kusaidia jamii yenye uhitaji maalum.

“Nawaomba wakazi wa mikoa ya Geita, Mwanza na Shinyanga kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha tamasha hilo,” alisema Msama.

Msama alisema kupitia viingilio vya tamasha hilo wanatarajia kutoa kipaumbele kwa wakazi wa mikoa itakayopitiwa na tamasha kwa baiskeli zaidi ya 100 za walemavu ambazo zitagawiwa mikoa mbalimbali.

Aidha Msama alisema waimbaji mbalimbali wamethibitisha kushiriki tamasha hilo ambao wanaendelea na mazoezi ya kujiweka sawa.

Naye Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Khamis Pembe alisema wanaendelea na mikakati ya kuimarisha ulinzi kwa wakazi wa mikoa hiyo.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.