ASKOFU KAMETA AWAKARIBISHA WATANZANIA TAMASHA LA PASAKA


Askofu wa Jimbo la Mashariki Kusini wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dk. Lawrence Kameta amewakaribisha Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye Tamasha la Pasaka litakalofanyika Kanda ya Ziwa kwa sababu limejikita kukemea maovu yaliyokuwa yakifanyika katika mikoa hiyo ambayo ni mauaji ya albino na vikongwe.

Askofu Kameta alisema Tamasha la Pasaka mwaka huu ni la kwanza kwa uongozi wa awamu ya tano ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye ameingia akiwa na kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.

Kwa mujibu wa Askofu wa Kametta kusudi la Sikukuu ya Pasaka ni kusherehekea kufufuka kwa Yesu Kristo ambaye ufufuko wake ni kuondokana na dhambi kwa wanadamu, hivyo ni nafasi ya pekee kwa wanadamu kurudisha shukrani zao.

“Kila mmoja anatakiwa kukubali kazi ya Msalaba ambayo itasaidia serikali hasa kutotumia nguvu zaidi katika majeshi yake kama Magereza, Jeshi la Wananchi (JWTZ) ili raia wote wawe wema katika kumtukuza na kumuabudu Mungu,” alisema Askofu Kametta.

Aidha Askofu Kametta alitumia fursa hiyo kuwaombea waliopitia kipindi kigumu cha maisha yao ikiwa ni wiki ya mwisho ya maombi kuelekea katika sikukuu ya Pasaka.

“Wiki ya mwisho ya kuelekea Pasaka, Watanzania tunatakiwa kuwaombea wenzetu waliopitia kipindi kigumu cha maisha duniani, tuwaombee ndugu zetu duniani,” alisema Askofu Kametta.

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka Alex Msama alisema maandalizi ya tamasha hilo yanakwenda vizuri kama walivyopanga.

Msama alitumia fursa hiyo kuitaja mikoa itakayopitiwa na tamasha hilo ni pamoja na Geita (Machi 26), Mwanza (Machi 27) na Kahama (Machi 28) ambako pia alitaja viingilio kwa wakubwa ni shilingi 5000 kwa wakubwa na shilingi 2000 kwa watoto
Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.