CHAGUO LA GK: NIKUFAHAMU KUTOKA KWA EVELYN WANJIRU


Tunatumaini u mzima mdau wetu wa Gospel Kitaa hasa kwa siku ya leo Jumapili tulivu yenye kuvutia na upako maradufu kiroho na kila nyanja katika maisha yetu. Kwa ujumla ni siku njema ya Bwana ambapo sisi kama watoto wake tunakutana kwa pamoja na kumpa sifa na utukufu.

Leo ikiwa ni Jumapili ya mitende ambayo huadhimishwa kila Jumapili ya mwisho kabla ya pasaka. Makanisa mbalimbali huwa na utaratibu wa kugawa matawi ya miti ya mitende au inayofanana na hiyo kuonyesha kumkaribisha Kristo Yesu katika mji mtakatifu wa Yerusalemu wakiimba nyimbo za shangwe na kupepea matawi ya miti wakiimba "Hosiana hosiana mbarikiwa asifiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana".

Basi yote yakiendelea sisi tunaanza siku na mwanadada kutoka nchini Kenya Evelyn Wanjiru na wimbo wake mzuri uliofanya vizuri katika anga la injili nchini Kenya uitwao, Nikufahamu. Wimbo huu umebeba ujumbe mzito sana ukiusikiliza utagundua kuwa katika Dunia ya sasa twatakiwa kumfahamu zaidi Mungu wetu aliye hai, tuwe na shauku ya kumjua zaidi yeye aliye juu mwenye mamlaka zaidi aliyebeba dhambi zetu na sasa tuko huru.
Tunachangua kumfahamu bwana na Evelyn Wanjiru katika jumapili hii ya mitende.Angalia video hii ya Nikufahamu bwana. 
 Tukutane wiki ijayo...
Share on Google Plus

About Desdery Charles

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.