CHAMUITA YAUNGA MKONO TAMASHA LA PASAKA

Na Mwandishi Wetu
Ado November ©Strictly Gospel
Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) imeunga mkono mpango wa tamasha la pasaka kuelekezwa kanda ya ziwa, kwa kufafanua kwamba kinachoenezwa ni Neno la Mungu na si huduma pekee kama inavyodhaniwa na jamii.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa CHAMUITA, Addo November ameelza kwamba kwa kuwa ni Neno la Mungu, ndio maana mwaka huu tamasha liko mikoa ya Kanda ya Ziwa na kuachana na Dar es Salaam kama ilivyozoeleka.

November alisema kuwa Msama ameonesha kwamba tamasha hilo ni sehemu ya huduma ametumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa mikoa ya Geita, Mwanza na Wilaya ya Kahama na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi ili kupata ujumbe wa neno la Mungu kutoka kwa waimbaji mbalimbali.

November alisema kampuni ya Msama imejipambanua kwamba kupitia tamasha la mwaka huu kuwasaidia walemavu ambao watakabidhiwa baiskeli zaidi ya 100.

Aidha naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema wanaendelea na mchakato wa kufanikisha ibada hiyo muhimu kupitia waimbaji na viongozi wa dini.

Msama alisema tamasha hilo linatarajia kuanza Machi 26 mkoani Geita, Machi 27 Mwanza na Kahama itakuwa Machi 28 ambako waimbaji mbalimbali wamethibitisha kushiriki katika tamasha hilo.

“Nawaomba wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha msaada kwa wenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu na wajane, hivyo wakazi wa mikoa wajitokeze,” alisema Msama.

Msama alisema viingilio katika tamasha hilo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na shilingi 2000 kwa watoto ambako waimbaji waliothibitisha kushiriki katika tamasha hilo ni Rose Muhando, Upendo Nkone, Bonny Mwaitege, Jesca BM, Joshua Mlelwa, Jenipher Mgendi, Faustin Munishi, Kwaya ya Wakorintho Wapili na Kwaya ya AIC Makongoro.
Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.