HABARI PICHA: MAZISHI YA MAMA FRIDA MWAMWAJA KUTOKA KYELA

Watoto wa marehemu pembeni ya kaburi ya mama yao
Hatimaye Jumamosi ya tarehe 19 Kyela, ndipo mwili wa Mama Frida Mwamwaja ulipumzishwa, baada ya kufariki tarehe 15 Machi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mama Frida amezaliwa tarehe 19 Disemba 1953, hivyo kufariki akiwa na umri wa miaka 62 akiacha watoto 3 wa kiume na mmoja wa kike, huku wajukuu wakiwa saba.

Kwa mujibu wa maelezo ya mtoto mmojawapo wa marehemu, kwa ghafla akiwa chumbani kwake alianza kusikia kizunguzungu, na baada ya hapo alianza kuomba na kisha alipomaliza alipata wakati mgumu kupumua na kisha kuanguka, kabla ya kuwahishwa hospitalini kwa ajili ya uangalizi zaidi, hadi hapo mauti ilipomfika.

Ambwene na kaka yake mkubwa Nelson wakiwa na bibi yao mzaa mama baada ya mazishiMama mzazi wa marehemu

Mchungaji Mwakasege wa Naioth Gospel Assembly


Mtoto wa tatu wa marehemu Ipyanamtoto wa mwisho wa marehemu

Mama mzazi wa marehemu


Watoto wa kiume wa marehemu  Ambwene, Ipyana pamoja na Atufi (Nelson)
Ksatika yote, hatuna cha zaidi ya kumtukuza Mungu kwa ukuu wake, maana atenda na kuwaza kwa muda wake tofauti na wanadamu. Tunaomba faraja ya Mungu iwe pamoja na wafiwa wote, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo.

BWANA ametoa na BWANA ametwaa, Jina la BWANA libarikiwe.
Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.