KONGAMANO LA MOYO WA MWANAMKE 2016 LAANZA LIVING WATER

Katika kuelekea Siku ya Wanawake Duniani, Kanisa la Living Water Centre Kawe kupitia huduma ya Wamama kanisani hapo ikiongozwa na mbeba maono Mwalimu Lilian Ndegi wameandaa Kongamano linalojulikana kama “Kongamano la Moyo wa  Mwanamke”

Kongamano hili ambalo hufanyika mara moja kila mwaka katika Kanisa la Living Water Centre Kawe chini ya mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi na Mwalimu Lilian Ndegi, hukusudia kuwajenga Wanawake kuwa na uwezo katika kumtumika Mungu na kujua nafasi yao ya kutumika aliyowapa katika ufalme Mungu.

Kaulimbiu ya mwaka huu ni; "Mwanamke Mjenzi" Mithali 14:1.

Kusudi kuu la kongamano ni kuwafanya wanawake kuwa watendaji katika ufalme wa Mungu na wawajibikaji na watekelezaji wa majukumu katika ngazi ya familia, huduma, jamii na taifa kwa ujumla.

Waimbaji mbalimbali ikiwemo Women of The Kingdom, Living Waters, More than Enough Band watakuwepo kuhudumu.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kutumia namba ifuatayo; 0713 580 400

Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.