MHE. PAUL MAKONDA AMSHUKURU MUNGU KUMUWEZESHA KAZINI

 Mh. Paul Makonda akiwa na Mke wake akimshukuru Mungu
Mhe. Paul Makonda siku ya Jumapili alikuwa anatimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe kuwa mkuu wa Walaya Kinondoni,asubuhi ya leo katika Ibada Kanisani Living Water Center Ministry Kawe alipolelewa kiroho na anapo abudu alikuja kumshukuru Mungu na kutoa sadaka ya shukrani kwa hatua ambayo amefika.

Katika Ibada hiyo Mh Paul Makonda aliongozana na mke wake; alipopewa kuzungumza alisema anamshukuru Mungu kwa kutimiza mwaka tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Wilaya Kinondoni akisema haikuwa rahisi kwake ila Mungu amemuwezesha. Makonda aliongeza kwa kusema "usishindwe kufanya mambo ya kimaendeleo kwa changamoto za kimazingira au chochote kama kwangu ambavyo imekuwa ikionekana"

Mapema akimkaribisha kuzungumza Mhe. Paul Makonda Kiongozi wa Kanisa hilo Apostle Onesmo Ndegi alikuwa anaelezea jinsi ambavyo amemlea kiroho Mh.Makonda hata kabla ya kuingia kuwa mtumishi wa serikali jinsi alivyokuwa mbunifu wa shughuli mbalimbali hivyo kinachofanyika leo sio kipya kwake.

Baada ya Ibada hiyo ya shukrani Bwana akatenda zaidi kwa kumfanya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Hongera Paul Makonda kwa kuteuliwa kuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mh. Paul Makonda alipokuwa akizungumza
Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre Kawe Apostle Onesmo Ndegi 
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre alipokuwa akiwaeleza waumini kuhusu Mh. Paul Makonda
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre alipokuwa akiwaeleza waumini kuhusu Mh. Paul Makonda

 Mh. Paul Makonda akiwa akifafanua jambo
Maombi yalifanyika kwake na mke wake ili Mungu amtangulie katika utumishi wake serikalini
Apostle Onesmo Ndegi, Mke wake Lilian Ndegi na Mch. Peace Matovu wakifanya maombi kwa Bwana na Bibi MakondaApostle Onesmo Ndegi,Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre Kawe akifanya maombi kwa watu waliokuja mbele kuokoka katika ibada hiyo
maombi kwa watu waliokuja mbele kuokoka katika ibada 

Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.