NDOTO YAKO HAIZUIWI NA UMRI, SONGA MBELE

Elie Chansa
GK Editor.
Bibi Cha  Sa-soon akifurahia ©Autosphere.fr
Kisa hiki kinatokana na tukio ambalo nimelisikia leo redioni, ati kwamba huyo bibi amekuwa akifuatilia leseni ya udereva kwa muda mrefu sana. Nikaona nimfuatilie, isitoshe kwa mbaali tuna undugu 😄😄

Miaka 6 iliyopita, Bibi Cha Sa-soon wa Seoul, Korea Kusini alikuwa mtu mwenye furaha sana, kwa maana alikabidhiwa cheti chake cha ufaulu, jambo lililomhalalishia kupewa leseni ya udereva.


Lakini furaha hiyo iliambatana na machozi na jasho la kutosha. Kwani katika historia, Bibi Cha alianza kuisaka leseni hiyo mnamo mwaka 2005. Lakini kwa miaka mitano mfululizo alifeli.

Labda nikuwekee kwa lugha nyepesi. Amefeli mara 960 kupata leseni. Na nikisema mara 960 ina maana amejaza fomu mara 960, amesailiwa mara 960, amepewa majibu mara 960, amesikitika mara 960 (maana nina hakika hakuna aliyefeli akafurahi), na mara zote hizo amesimamia ndoto yake. Amesimamia kile anachoamini, ya kwamba IPO SIKU!

Bibi Cha Sa-soon akionesga cheti cha ufaulu ©motortrivia.com
Kukurasishia zaidi ni kwamba Bibi Cha Sa-soon amewekeza mara 960 katika malengo yake, na wala hajaangalia muda gani imemgharimu. Gharama kubwa kwake ni kushindwa kufanikiwa. Amethubutu kwa miaka mitano hadi akathibitishwa. Wewe umejaribu mara ngapi?

Ni juzi tu ofisini kwangu alipita mdada mmoja akanieleza namna ambavyo ameapply kazi sehemu. Nafasi za kazo zilipotangazwa, hakulala, aliapply nafasi 11 kati ya 12 zilizotangazwa, na kati ya zote hizo akaitwa kwenye nafasi mbili. Aliwaza mbele zaidi, aliwaza mbali zaidi.

Huwa kuna mfano niliwahi kumpa rafiki yangu mmoja studio. Namshukuru Mungu ulimsaidia.
Mfano wa ukataji tamaa pasi na kuua kilicho mbele
'wewe kama umejaribu mara zote hizo ukaona kama mambo ni magumu na ukaamua kuacha, poa. Acha tu kafanye issue nyingine. Lakini tambua kwamba majaribio yako yote ni kama jitihada za kufungua mlango ukiojiloki. Umejaribi mara kumi ukahiso labda mlango huo katu hauwezi kufunguka, ukaondoka. Bila kujua kwamba ulichofanya wewe ni kurahisisha kazi ya mwingine kwa namna ulivyokata tamaa. Atafika mtu mwingine na. Kuugusa kidpogo tu huo mlango na utafunguka, kwa sababu tu uliishia njiani ukachoka. Na iwapo ungesonga kidogo tu basi ungeshafungua mlango na kuingia ndani"

Na hiyo ni kwako pia. Kama unadhani mara tatu ulizojaribu zinatosha, basi UNACHEKESHA. Cha Sa-soon kawekeza mara 960. Mimi hata mara 50 sijafika. Na umri wenyewe hata hauna kikwazo.. naam hauna kikwazo maana Cha ameanza kutafuta leseni akiwa na umri wa miaka 64. Na akaipata akiwa na umri wa miaka 69, na hatimaye gari yake ikaanza kuendeshwa naye mwenyewe kwenye shughuli za kuuza mbogamboga.

Wewe uko kwenye jaribio la ngapi? BWANA Yesu akupe wepesei wa kusonga mbele zaidi.

Nikumbushe siku nyingine nikueleze habari ya ku-"act like an immigrant"

Elie@inhouse.co.tz
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.