SHANGWE ZA GK: USIKU WA RONNIE NA SAADA


Katika Shangwe za GK leo ni usiku maalum wa Ronnie na Saada ndani ya ukumbi wa Shekinnar Garden, Mbezi Beach.

Tofuati na harusi zingine ni kwamba hii iliongozwa kwa Lugha ya Kiingereza kwa sababu Bwana Harusi hajui lugha ya Kiswahili, huku Bibi Harusi yeye akijua kidogo, na hata hadhira iliyokuwepo pia ikapelekea tukio kushereheshwa na mtaalamu wa mawasiliano ya umma, MC Lawrence Mwantimwa.

Tukio lilijawa watu wenye furaha mwanzo hadi mwisho wa sherehe na hata kufikia kamati kuomba muda wa nyongeza "extra time" ili vinywaji vipate wanywaji kutokana na kusheheni maboksi kwa maboksi, na kreti kwa kreti.

Kutokana na ombi kuridhiwa, sherehe ikatamatika rasmi saa tano usiku kwa udhamini wa Mwanti Car Trade na Gospel Kitaa.

Zifuatazo ni picha kadhaa za tukio...


Mtu na mkewe.

MC Lawrence na Mhe Balozi wa Zambia, Judith KapinimpaShare on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.