TAARIFA KWA UMMA: KUTOWEKA KWA MWANDISHI SALMA SAID

salma
Mwandishi Bi. Salma Said.

TAARIFA KWA UMMA
KUTOWEKA KWA MWANDISHI SALMA SAID

Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen na MwanaSpoti, inaendelea kufuatilia kwa makini kutoweka kwa Mwandishi wetu wa Zanzibar, Bi Salma Said.

Taarifa za kutoweka kwa Bi Salma zilitufikia Ijumaa mchana tarehe 18 Machi 2016 kupitia kwa mume wake. Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote inayoonyesha ni nani au chombo gani kinamshikilia au kumhifadhi.

Hali hii inatutia wasiwasi mkubwa kama kampuni na wadau wa habari. Tunachukua fursa hii kuvitaka vyombo vya dola – vyenye dhamana ya ulinzi na usalama wa raia wake – kulitafutia ufumbuzi wa haraka suala hili ili kumaliza utata uliozingira kutoweka kwa Mwandishi Salma.

Imetolewa na
Francis M. Nanai
Mkurugenzi Mtendaji,
Mwananchi Communications Ltd
20.03.2016
Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.