MUISLAMU AUWAWA BAADA YA KUWATAKIA HERI YA PASAKA WAKRISTO

Marehemu Asad Shah ©ChristianPost
Katika hali ambayo inatafsiriwa kuwa ni chuki baina ya wafuasi wa dini ya kiislamu na wale wa Kikristo, Bwana mmoja nchini Scotland ameuwawa kwa kuchomwa kisu, kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kuwatakia heri wafuasi ya dini ya Kikristo katika msimu wa pasaka.

Asad Shah mwenye umri wa miaka 40 amekutwa na umauti masaa machache baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa facebook tarehe 24 Machi kuhusiana na sikukuu ya pasaka, ambapo Wakristo duniani huadhimisha kufa na kufufuka kwa BWANA na Mwokozi wao, Yesu Kristo.

Mashada kumuenzi Asad. Moja ya picha iliyopo kwenye tovuti ya kumuenzi ©Asad Shah Memorial
Mara baada ya tukio hilo kutokea, baadhi ya wateja wa Shah ambao wamekuwa wakifanya manunuzi kwenye duka analofanya kazi, walijitokeza na kuandaa utaratibu wa kuchangishana pesa kwa ajili ya gharama za mazishi na hata kwa familia kufanya kitu chochote ambacho wangependa kufanyia kwa kiwango watakachokabidhiwa.

Tofauti na matarajio ya kutafuta pauni 1,500 ambayo ni sawa na takribani shilingi milioni 4 na nusu kwa fedha Tanzania, kiasi kilichochangwa kimezidi kwa zaidi yamara sabini, na kufikia takribani pauni laki moja na kumi na moja, sawa na zaidi ya shilingi milioni 340; kiasi ambacho kimechangwa na watu elfu 5 hadi hdi hivi sasa.

Picha kutoka tovuti inayokusanya fedha za kusaidia familia ya marehemu ©gofundme
Kwa mujibu wa tamko ambalo limetolewa na familia na kushuhudiwa na GK, sikuzote Shah amekuwa mwenye kuheshimu watu wote bila kuangalia asili yake, bali kuwaona wote kama wanadamu walio sawasawa.

Hata hivyo pamoja na kuaminika kwamba chanzo cha kifo chake kinatokana na kuwatakia heri wakristo, baadhi ya fununu zinaeleza kwamba Shah amekuwa akipokea vitisho vya aina mbalimbali kutokana na baadhi ya waislamu wenye msimamo mkali kuamini kwamba yeye ni nabii wa uongo.

Kwa mujibu wa kiongozi wa msikiti wa Glasgow Ahmadi, Bwana Owusu Konadu, ameeleza kwamba iwapo Shah angetoa taarifa mapema kwenye kwa uongozi wa msikiti huo, basi nao wangelifikisha taarifa hizo polisi ili zipate kufanyiwa kazi, lakini aliamua kuwa kimya.

Taarifa za kutishiwa zimepatikana baada ya rafiki wa marehemu kupitia kurasa zake za kijamii na hivyo kuona kilichokuwa kinaendelea. Hata hivyo bado inaaminika kwamba upendo wake kwa kila mtu ndio umepelekea mauti yake.

Christian Post imeandika
Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.