NJOO TUONYESHANE VIPAJI TAR 10 T.A.G PATANDI, ARUSHA

Kusudi la Kristo ndani ya vijana kupitia kile ambacho wanapenda.


Praise and worship imekuwepo kwa sana Jijini Arusha, hii imekuwa inatimiza lengo la kumtukuza Mungu. Lakini kumekuwa na wale wengine wa nje ambao wanahitaji kufikiwa, wawe activated ili nao wapate sehemu ndani ya mwili wa Kristo.

Wengi wa vijana wamekuwa wanadhani kwamba wakishaokoka basi ni mwendo wa kuchomokea mashati juu karibu na kifua. Na kwamba ubunifu wao kwa kazi wanazofanya zitakwisha na kupotea mara baada ya kuokoka.

Tukio la Rap Battle limekuja kufuta hiyo dhana, na ili kuwafahamisha vijana wote kwamba kwa chochote kipaji walichobarikiwa nacho kwayo, basi kinaweza kutumika kwa ajili ya utukufu wa Mungu na hata kuwavuta wengineo ili Mbinguni tuingie kwa pamoja.

Njoo wewe na mwenzako, andaa mistari utakayochana, kisha usikie upande wa pili wakichana kueleza uzuri wa Yesu, umuhimu wake na fadhili zake zilizo za milele. Pamoja na nayo, kuna kuonyeshana ubabe wa kucheza, halafu mwisho wa siku na tusadiki, ya kwamba Yesu ndiye aliyetufia msalabani, na kufufuka siku ya tatu, na kwamba ndiye Mwamba na Mwokozi wetu.

Tukutane Jumapili tarehe 10 Aprili 2016 ndani ya T.A.G Patandi kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na mbili jioni.

Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.