SNOOP DOGG DOGG ASEMA NI HERI KUWA NA YESU KULIKO FEDHA NA DHAHABU

Snoop Dogg Dogg ©Mirror
Mwimbaji wa muziki maarufu wa kufokafoka ama rap kama unavyojulikana duniani aitwaye Calvin Cordozar Broadus, Jr au maarufu kwa jina lake la kimuziki Dogg amewaachia tabasamu kuu baadhi ya mashabiki wake na wapenzi wa muziki wa injili kuhusu hatua yake ya kuimba kipande cha wimbo "ni bora kuwa na Yesu kuliko fedha ama dhahabu" "I'd rather have Jesus than silver and gold.

Mfokaji huyo aliweka kipande hicho katika anuani yake ya Instagram wimbo ambao ulikuwa ukipigwa redioni nayeye akifuatilia kwa kuuimba. Ambapo kati ya pongezi alizopata kutoka kwa wanaomfuatilia kwenye anuani yake hiyo zaidi zilikuwa pongezi kwake kwa hatua hiyo hasa ikijulikana kwamba mwimbaji huyo katika nyimbo na video zake amekuwa na kawaida ya kutumia picha zenye muashilio wa ngono na madawa ya kulevya lakini kwa kuonyesha kipande hicho akimsifu Mungu ilikuwa ni habari njema kwa wanaomuombea.

Tazama mfokaji huyo akiimba katika video hiyo kwa kubonyeza Hapa 


Sikiliza sauti ya wimbo huo hapa chini kama ulivyoimbwa na Kirk Franklin
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.