SOMO: JAMBO LA KUFANYA MAMBO YAKO YANAPOHARIBIKA (2)


Jumatano iliyopita pamoja na kupata utangulizi wa somo hili, tulijifunza vitu muhimu vitakavyokusaidia kutatua tatizo lako na kukutoa pale ulipo. Unaweza kusoma kwa kubofya hapa. Kisha ndipo tuendelee na sehemu ya pili ya somo letu; kutafuta chanzo cha tatizo lako.

Mwalimu Kelvin Kitaso
TAFUTA NINI CHANZO CHA TATIZO LAKO
“Huwezi kutibu ugonjwa kama hujui chanzo cha ugonjwa”
Luka 15:18, “Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako.”
2 Wafalme 6:6 “Mtu wa Mungu akasema, kilianguka wapi? Akamwonyesha mahali. Akakata kijiti, akakitupa pale pale, chuma kikaelea.”
Ufunuo 2:5 “Basi kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo naja kwako, name nitakiondoa kinara chako mahali pake, usipotubu.”
Ukifahamu nini chanzo cha kushindwa kwako ni lazima uwe katika uwezo wa kutatua tatizo.
Ukitaka kukata mti ili usiote tena ni lazima uchimbe chini na kutoa mizizi yake yote pale ulipoanzia kuota, hapo utamudu uhai wa huo mti na itabaki historia kuwa mahali Fulani palikuwa na mti wakati Fulani ila sasa haupo tena. Ukiwa na dhana ya kukata mti lakini ukawa unakata matawi tu ni lazima utakuwa unajisumbua bure tu na kupoteza muda wako bure kwa kuwa kwa kufanya hivyo ni lazima yataota mengi zaidi ya yale ya kwanza. Usiangaike na matawi geuka na uanze kuhangaika na shina.
Hta kama ni katika biashara yako au mambo ya familia yako au mahusiano yako na Mungu yanaenda vibaya, wewe kumbuka kutafuta chanzo cha matatizo na si kuangaika na kukata matawi.
“Usiangaike na matokeo, angaika na chanzo cha hayo matokeo”
Namfahamu mama mmoja ambaye alikuwa akiishi katika mgogoro wa muda mrefu sana na mume wake na kila wakati alikuwa akipishana sana na mume wake na kushindana nae kwa maneno makali. Hali ile ilisababisha ndoa yao kuwa yamoto kama kuzimu ndogo, ikamlazimu yule baba aanze kurudi usiku sana akikwepa makelele ya yule mke na kuamka na kuondoka mapema. Katika harakati za kimaisha yule mwanamume alikutana na kimada ambaye alikuwa akimfariji sana na kuwa kama mke kwake katika kila wakati alipokutana naye. Yule mke halali alipofahamu haya alikuwa akiumia sana moyoni mwake, alipoamua kuzingatia moyoni mwake aligundua kuwa chanzo zha matatizo ni yeye mwenyewe kuna kitu ameshindwa kukifanya kama mke, ndipo alipoamua kugeuka na kujirekebisha, ndipo alipoona yule mume wake anarudi tena na kumpata kama ilivyokuwa mwanzoni mwa ndoa yao.
Ni vyema kufahamu kuwa kujua chanzo cha tatizo ni mwanzo wa kutatua tatizo.
Kuna vitu ambavyo umfanya mtu kutoona chanzo cha tatizo, ambavyo umfunga mtu asipate kuona kabisa chanzo cha tatizo,  vitu hivyo ni kama:-
1.     Kutoshituka.
Kuwa na hali ya kuona ni kawaida tu, kumbuka kuwa mwana mpotevu aligundua tatizo baada ya kushituka tu kuwa mambo hayaendi sawa. Ni lazima ushituke kuwa hiyo hali uliyonayo si wewe halisi.
2.     Kutochoka matokeo ya tatizo.
Kama haujachoka mambo yanavyoenda ni lazima usigundue chanzo cha tatizo.
3.     Kukata tamaa kulikokithiri.
Ukikata tama asana hautoweza kulikabili tatizo wala kujua chanzo chake.
4.     Kulidhika na hali uliyonayo
5.     Kujitia moyo kuwa hilo ni jaribu tu unapitishwa.
Yakobo 1:13 “Mtu ajaribiwapo, asiseme, ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu”
Kuna watu hupenda kumsingizia Mungu kuwa anawapitisha kwenye matatizo ambayo wao wenyewe ndiyo chanzo cha hayo matatizo. Mungu hawezi kumjaribu mtu katika mambo ya kuharibu, yeye yupo katika mambo yajengayo. Ni lazima ukumbuke wapi ulipoanguka na ukatubu.
6.      Kulaumu laumu wengine katika tatizo lako.
Kulaumu uonekana ni kuzuri kwa kuwa kunakusaidia kushusha mzigo uliopo moyoni kwa wakati huo tu, ila hakuondoi tatizo kabisa bali uzidisha tatizo kwa kuwa utadhani umenawa kumbe tatizo lipo palepale.
Ukitaka kuona tatizo linaendelea upande wako ni lazima ujifunze tabia hii ya kulaumu.
Mfano msuri ni mfano wa Adamu na Hawa kwa kulaumu kwao hawakuweza kutatua tatizo lililokuwepo wala hawakubaini chanzo cha tatizo ni nini. Ubaya wa kulaumu unaleta uwezekana wa wewe kurudia tatizo hilo hilo mara kwa mara kwa kuwa hujui chanzo.
7.     Kutojali tatizo/kudharau tatizo.
Tabia hii hupelekea pia kutochukua hatua za msingi.
8.     Kujiona kuwa wewe si sehemu ya tatizo/kukwepa tatizo.
9.     Kutotaka kushuka
Luka 15:19 “Sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.”
Jaribu kufikilia kama mwana mpotevu asingetaka kushuka nini kingetokea?  Viburi na kutotaka kushuka na hata kuelekezwa vinapofushwa macho ya watu kutoona chanzo cha tatizo.
Ukitazama pia mfano wa nyumba, nyumba ni msingi, msingi ukiwa mbovu basi nyumba hiyo uhai wake hautakuwa salama, ila kama msingi ni imara basi nyumba pia itakuwa imara sana. Kama unakusudia kuibomoa nyumba isionekane tena ni lazima uende kwenye msingi wake na ukabomoe msingi kwanza. Mfano huu ni wakuzingatia sana hata kwa wazazi wa kiroho ni lazima wajitahabishe kuwajengea washirika wao misingi iliyo imara ambayo itawasaidia kuwa imara katika wokovu. Ni ukweli usiopingika kuwa walokole wengi huwa wakristo wa kawaida na waliodhaifu kupambana vita vya kiroho kwa sababu wengi wao hawajaandaliwa vyema katika msingi na kama waliandaliwa basi misingi hiyo tayari imeharibika.
Zaburi 11:3 “Kama misingi ikiharibika, mwenye haki atafanya nini?”
Maandiko huonyesha kwa wazi sana tatizo huwa ni misingi kama ikiharibika mwenye haki huwa katika wakati mgumu na wakati mwingine naye huweza haribika na kujikuta kazama na kuingia katika mifumo mibovu. Msingi ni chanzo cha jingo kuwepo, kwa hiyo kama jingo husumbua anza kuangalia katika msingi kuna nini kimeharibika au ni nini chanzo cha jingo hilo kusumbua kwa namna hiyo.
Mwalimu Kelvin Kitaso anapatikana kupitia 0767190019 / 0713804078 na pia kupitia barua pepe; kitasokelvin@gmail.comShare on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.