SOMO: KUFUNGA VIWANDA VYA UHARIBIFU - ASKOFU GWAJIMA

Askofu Mkuu Josephat Gwajima Kanisa la Ufufuo na Uzima Duniani

KUFUNGA VIWANDA VYA UHARIBIFU

Kila jambo unaloliona duniani liwe zuri au baya linaanzia kwenye ulimwengu wa r oho. Kuna ulimwengu usioonekana kwa macho unaitwa ulimwengu wa roho na kuna ulimwengu wa mwili. Lolote lililokupata kama hukushinda kwenye ulimwengu wa roho litarudi tena kukupata. Vipo viwanda kwenye ulimwengu wa rohoni vinavyotengenezwa viachie dhiki duniani. Vipo vya kuzalisha ajali, kuzalisha kansa, kuzalisha umaskini, kuzalisha balaa na mikosi n.k


Waefeso1: 3 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo”.

Waefeso 1: 20 “Aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho”.

Baraka zetu zinaanzia rohoni na kudhihirika mwilini. Kuna roho anatenda kazi ya kuharibu ndoa, matatizo, taabu, ajali, wizi. Huyu ndiye anatengeneza matatizo hayo, kiwanda hiki kikifungwa bidhaa za mikosi, balaa, matatizo, ajali na matatizo mengine yote hazitoki tena.

Waefeso 3: 10 “ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho”

Waefeso 6: 12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”
Wapo wafalme, zipo mamlaka, wapo wakuu wa nguvu za giza, yapo majeshi ya pepo wabaya, wapo wanaokaa kwenye ulimwengu roho ambao wanatengeneza mtiririko wa matatizo ambao unadhaniwa ni asili ya wanadamu. Lazima viwanda hivi vya matatizo vifungwe rohoni kwa jina la Yesu. Ukifunga kiwanda cha rohoni mumeo anapatikana, kazi inapatikana, kampuni inapatikana, safari inapatikana. Unayoyaona yanatokea mwilini na kila tukio linalokupata limetengenezwa mahali rohoni. Funga kiwanda kinachokuletea udhaifu, kipo kiwanda kinachokuletea magonjwa na kukataliwa kifunge kwa jina la Yesu.

Ayubu 1:1 1 “Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu. Kisha walizaliwa kwake wana saba, na binti watatu. Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki. Nao wanawe huenda na kufanya karamu katika nyumba ya kila mmoja wao kwa siku yake; nao wakatuma na kuwaita maumbu yao watatu ili waje kula na kunywa pamoja nao. Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote. Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako. Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana. Ilitukia siku moja hao wanawe na binti zake walipokuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa, mjumbe akamfikilia Ayubu na kumwambia, Hao ng'ombe walikuwa wakilima, na punda walikuwa wakilisha karibu nao; mara Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua hao watumishi kwa makali ya upanga, mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wanao na binti zako walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa; mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia; akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe. Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu.”

Mungu ametuonyesha hapa kabla ya kuona tatizo lililompata Ayubu anatuonyesha familia yake ya watoto kumi na anamcha Bwana. Anatuonyesha na utajiri wake wa kondoo ambao walikuwa elfu saba na ngamia elfu tatu na jozi za ng’ombe mia tano(Elfu moja), punda mia tano (punda walikuwa wanatumika kama usafiri) na watu wengi sana wa nyumbani kwake na alikuwa mkuu kuliko watu wote wa upande wa mashariki.

Ayubu1: 7 "Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo."

Mungu akaanzisha mazungumzo na shetani ili atufundishe kwamba kuna viwanda vya kushughulikia. Lakini shetani alimshawishi Mungu aunyooshe mkono wake ili amharibie, lakini Mungu kwasababu sio Mungu wa kuharibi alimjibu shetani kwamba yote Ayubu aliyonayo yamo katika uweza wake(shetani) hivyo aviguse lakini kwenye uzima wake asiweke kidole na wakati huo Ayubu hakufahamu mazungumzo hayo yote, Tunajifunza shetani anauweza wa kugusa kwenye maisha yetu na yapo mazungumzo mabaya huwa yanafanyika kwa siri juu yetu lakini hatuogopi kwasababu Mungu yupo upande wetu na hakuna aliye juu yetu.

Tumeona baada ya yale mazungumzo ya rohoni kiwanda cha ujambazi kikafyatua tukio la wizi likatokea mwilini na wezi wale wakawa na jina (waseba) tukio hili linaoneka la kawaida lakini limeanzia rohoni, ng’ombe elfu mbili na punda mia tano wote wameondoka kwa mara moja, tunajifunza matukio yanaweza kuja kwa mara moja mfululizo.

Wengine wakatokea na kusema ni moto wa Mungu lakini sio, unasikia watu wanasema ni kazi ya mwenyezi Mungu, dunia imetengenezwa kupeana faraja.

Tukio la tatu lililompata Ayubu. Shetani amefanya kitu kwenye ulimwengu wa roho wakatokea wakaldayo waliowauwa wafanyakazi wa ayubu akabakia mmoja wa kupeleka taarifa. Inawezekana na wewe kazini au familia wanakuchukia wote na unajiuliza Baba, dada, mama hanipendi kwa nini kumbe wametengenezwa wale kwenye ulimwengu wa rohoni.
Tukio la nne lilompata Ayubu ni upepo uliotokea jangwani ukaipiga nyumba yake pande zote na kuwauwa watoto wake akabakia mtu mmoja wa kuleta habari.

Lazima ujue kukifuata kiwanda mahali kilipo na ukivunje kwasababu wewe ni Rungu la Bwana na silaha za Bwana za Vita, kwa wewe utavunjavunja mwanamke na mwanaume, kwa wewe utavunjavunja gari la vita na waliochukuliwa ndani yake. Simama usilalamike tafuta mahali kilipo kiwanda chako ukibomoe na utapata vyote unavyovitaka kwa jina la Yesu”

Kiwanda cha kutengeneza uzinzi kikilipua unazini japo hutaki, kiwanda cha kutengeneza mikosi kikilipua mikosi inakufuata unabaki unalalamika na kushangaa, unatakiwa ujue vipo rohoni viwanda hivyo uvivunje kwa jina la Yesu.

Kwenye matukio haya tumeona kuna majambazi, upepo, na moto vimempata Ayubu,hivi vimeanzia vimeanzia rohoni. Kumbe kuna matukio kama ya matetemeko, wizi, moto, ajali yanayotokea kwenye maisha yako chanzo chake ni rohoni.

Isaya19: 18 “Katika siku hiyo itakuwako miji mitano katika nchi ya Misri itumiayo lugha ya Kanaani, na kumwapia Bwana wa majeshi; mji mmoja utaitwa Mji wa uharibifu.”

Ipo miji ambayo kazi yake ni kutengeneza uharibifu, na ndani yake yupo malaika wa uharibifu. Linatengenezwa jambo likupate mpaka uharibikiwe

Ufunuo wa Yohana 9:11 “Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.”

Ukiri:-
“Kwa jina la Yesu kiwanda kilichojengwa kwaajili ya familia yangu nakiharibu kwa jina la Yesu kiwanda kilichotengenezwa juu ya maisha yangu nakiteketeza kwa jina Yesu, ”

Kuna vitu vimetengenezwa kuharibu maisha yako kwa uzinzi, magonjwa, umaskini, kuachwa, talaka, tukio la kuharibu mimba Unawaza mbona mimi kila siku kumbe umetenengenezwa. Kuna kuzimu ya baharini na kuzimu ya nchi(nikamwona mnyama akitoka katika nchi),kuna kuzimu ndogondogo za wachawi zimetenegenezwa ziharibu watu. Ile akili sio ya kwako, imetenegenezwa ili uwe

Wafanyakazi wa viwanda hivi ni wachawi, waganga wa kienyeji, wasoma nyota na wengineo na bidhaa zao ni kansa, mikosi, balaa, ajali, kukataliwa, uoga, kukata tamaa, kujichukia, kokosa kazi. Shambulia viwanda hivyo na bidhaa zao zisizalishwe tena uwe huru kwa jina la Yesu.

“ Kwa jina la Yesu kristo ninavunja kiwanda cha ajali, kiwanda cha magonjwa, kiwanda cha kukataliwa, kiwanda cha kuzalisha balaa na mikosi, ninateketeza kwa damu ya Yesu, kwa jina la Yesu ninavunja viwanda vyote vilivyoshikia familia yangu kwa jina la Yesu, ninavunja viwanda vya kuzalisha majambazi, moto wa kishetani na matukio ya kishetani ninaviharibu kwa jina la Yesu. Amen


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.