TAARIFA KWA VIJANA: TANZANIA NATIONAL YOUTH ASSEMBLYTunapenda kuwa taarifu kwamba, Kongamano letu litaanza saa mbili ahsubuhi hadi saa kumi na moja jioni kwa siku zote mbili, yaani Juma mosi na Juma Pili, tarehe 9-10 April, katika Ukumbi wa Sundown Carnival Hotel.

Idadi ya Vijana tunaowatarajia kuwapokea kwa mujibu wa data zetu hadi kufikia usiku huu wa tarehe 5 April 2016, ni Vijana 843, wakiwa wametokea mikoa yote Tanzania, na nchi jirani ya Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.   Tunapenda kuwakaribisha nyote katika Jiji la Arusha.


Pia, kiingilio imefanywa kuwa BURE kwa kila mshiriki, kutokana na juhudi za kamati kufanikisha kupata Wadhamini walioweza kulipia kiingilio cha zaidi ya washiriki 400, hasa kushiriki katika mafunzo hayo ndani ya ukumbi wa Sundown, uliopo pale Kisongo mita kama mia moja kabla ya tembo club ukiwa unatokea Arusha mjini.

Kwa wale wote waliolipia, na kutumiwa ticket zao, tunaomba waje na ticket zao siku hizo.

Halikadhalika, Hakuna kijana yoyote atayerudishwa getini kunyimwa kushiriki katika Kongamano hili muhimu kwa Vijana, hivyo bado tunatazamia, idadi zaidi ya 1000 ya Vijana kushiriki.

Tunasikitika kwamba kwa sasa hatupokei tena pesa ya mshiriki kwa ajili ya Chakula chake cha mchana, badala yake mtu atajigharamia mwenyewe akiwa hapo Hotelini.

Gharama za Vyeti, italipiwa na mshiriki Ukumbini.

Kwa niaba ya Kamati nzima ya maandalizi ya Tanzania National Youth Assembly, tunawakaribisha vijana wote bila kujali itakadi zetu katika jukwaa hili huru la Kujadili na kutoa suluhisho la kudumu la matatizo na changamoto zinazokabili jamii zetu, kwa mustakabali wa kizazi hiki na kizazi kijacho.

Agenda zetu zinapatikana kwenye tovuti yetu ya www.vijanaassembly.org ama utupigie kwa kupitia 0766075353 muda wowote.

NB: Tanzania National Youth Assembly siyo jukwaa la kisiasa, na wala haiegemei falsafa ya chama chochote ama dini yoyote, Bali ni Jukwaa huru la kujenga Umoja, Mshikamano na kujenga mtandao wa Vijana nchi nzima lenye lengo kubwa la kupeleka Taifa letu mbele kimaendeleo.

Lengo letu kuu ni kuleta mawazo mapya yenye kukuza Ubunifu kwa Vijana wote hasa katika nyanja zao husika.

Tunawatakia maandalizi mema.

Mbayani Tayai
M/kiti kamati ya Maandalizi,
Tanzania National Youth Assembly phase 1,
Arusha Tanzania.

Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.