TAMASHA LA MIC ON GOSPEL HIP HOP LILIVYOFANYIKA KATIKA PICHA

Hata picha ya pamoja nayo ina freestyle
Siku na saa zilisubiriwa, na hatimaye kutimia, ikashuhudiwa namna ambavyo vijana walijitokeza katika tukio la Mic On, Gospel Hip Hop, lililofanyika Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Patandi.

Tamasha hili la kipekee ambalo halijawai tokea lilihusisha makundi ya vijana waamini na wale wasioamini, ambapo kazi kubwa ilikuwa ni kueneza neno la Mungu kupitia vipaji vyao aina mbalimbali katika juhudi za kuwabadili vijana walio nje ya kanisa, kusudi wapate kujiunga kwenye boma la kueneza habari njema za Yesu, kupitia vipaji walivyotubukiwa.

Pamoja na kujitokeza kwa vijana wengi, waandaaji wanaeleza kwamba changamoto kubwa imetokana na vijana wa nje kuogopa kuingia ndani ya kanisa. Lakini tukio limefanikiwa kwa asilimia 75, hivyo kuona haja ya kulifanya kila mwezi, likihusisha semina na mafundisho kadha wa kadha kutokana na uhitaji na mwitikio mkubwa wa nje.

Zifuatazo ni picha za matukio kama ambavyo Gospel Kitaa inakuletea.

tafakuri

Mratibu wa shughuli, Douglas Kyungay
Mchungaji Daniel Kyungay


FDG Dancers
Mwalimu Shemeji Melayeki naye alipata wasaa wa kuwasihi vijana kutokuwa wepesi wa kukata tamaa.

Mnene Makweta

Novic

Sniper

DolaaJohn Maulid wa GKHata picha ya pamoja nayo ina freestyle


Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.