UJUMBE: VITA YA MASOLO KWENYE KWAYA (1&2) - MWALIMU JOHN MTANGOO

Bahati na Lydia kati ya mfano wa masolo mahiri nchini wanaoimba kwaya moja wakiwa na upendo wa hali ya juu ©CVC
VITA YA MASOLO
PART 1. CHANZO CHA TATIZO

Mungu alipoumba ulimwengu aliumba vitu viwili vya kudumu ili kuufanya ulimwengu uishi. Mosi CHAKULA Pili MUZIKI. Hivi vitu viwili vinadumu milele sawa na Neno la Mungu.
Muziki umekuwa na sifa kuu sana Duniani. Mpaka sasa sijakutana na mtu asiyependa muziki. Mungu wetu anakaa katika kiti cha sifa. Kwa sababu sisi tumeumbwa kwa sura na mfano wake basi tumechukua asili hii ya sifa. 
Japo inachukuliwa kama kupenda sifa ni utimilifu wa kibinadamu lakini asili hii shetani ameigeuza kutoka kwenye kusudi jema mpaka kuwa sehemu ya uharibifu wa kusudi la Mungu kwa wanadamu. 

Kwa hiyo CHANZO CHA TATIZO LA MASOLO NA UGOMVI NA KIBURI NI SABABU YA KUTAFUTA SIFA ZISIZO KATIKA MISINGI YA MUNGU.
Ikitokea kwaya fulani ina solo mmoja na hasa wa kike tegemea yafuatayo
1. Majibu ya hovyohovyo
2. Kiburi na ujuaji
3. Kuchelewa zoezi na ibadani
4. Wakati mwingine hapendi kufanana na wenzake(sare)
5. Ukahaba
Sasa kwa walio wengi na hasa wadada huonea wivu ama kukereka na tabia hizo ovu.
Nasema huona wivu sababu ukimfundisha solo mwingine mara nyingi anaiga tabia hizo. Nasema kukereka sababu wengi hutak wasolo ili wamkomoe yule mringaji hivyo kuongeza ukubwa wa tatizo. Kwa wale wanao muonea wivu hutamani nao kuwa maarufu na kupata sifa anazopata mwenzao. Hapa ndipo pagumu. 

UGOMVI MWINGI WA MASOLO UNALENGA ZAIDI KWENYE SIFA ZA KIBINADAMU KULIKO SIFA ZA MUNGU. HAPA NDIPO TATIZO HUANZIA.

PART 2. KULIELEWA TATIZO

Ili kutatua tatizo hili lazima kulielewa msingi wake. HUwezi tatua bila kuangalia eneo la vipaji ambalo ndio msingi wa changamoto zenyewe.
Kuna aina mbili za vipaji
1. vipaji vya kuzaliwa
2. Vipaji vya kutengenezwa.
Wale wenye vipaji vya asili vya kuzaliwa wana asili ya kuwa wapole na waelewa na ndio wanaongoza kwa kumsikiliza mwalimu. Mara nyingi sana mwalimu huwa hana kipaji kumzidi mwanafunzi wake lakini mwalimu anakuwa na ubongo wenye uelewa mpana kuliko mwanafunzi mwenye kipaji hivyo kupelekea mwanafunzi mwenye kipaji kutamani sana uelewa ulioko ndani ya mwalimu wake.Hapa ndipo Mungu aliweka usawa hasa. Hata kwenye kuimba mara chache sana utakutana na mwanafunzi mwenye kipaji mwenye kiburi. Wako wenye kipaji na kiburi na ni wachache sana lakini maisha yao kwenye uimbaji huwa mafupi sana. Wengi hujikuta wametolewa kwenye msitari wa uimbaji na mambo ya nje hivyo mwishoni hupokea dharau tu.
Wale wenye vipaji vya kutengenezwa ndio matatizo yote yamelala kwao.Mwenye ufahamu mdogo angependa dunia nzima ijue kama anajua. Unajua anaejua haitaji kujitangaza maana anajua mtajua kwamba anajua shida ni kwa asiyejua anavyotamani watu wajue kwamba anajua. Ndipo msingi wa part 1 unakuja KUTAFUTA SIFA KWA AJILI YA MAMBO BINAFSI NA SIO UTUKUFU WA MUNGU.
hata walimu wako makundi mawili kuna wenye vipaji vya asili vya kufundisha na kuna ambao mazingira yamewakuta kwenye nafasi ya kufundisha basi wanalisongesha gurudumu la uimbaji. Nimekutana na walimu wenye kiburi nami huwa nacheka sana maana ukikutana na mwalimu mwenye kiburi na masifa ujue hajui kitu huyo.

Kwa kawaida miziki iko ya aina nyingi sana na hakuna mtu ambaye anaweza kuimba kila aina ya mziki Duniani hivyo upana wa mwalimu kuandaa aina tofauti za miziki itapanua upana wa kutengeneza masolo wapya.Kama mwalimu anafundisha aina moja ya mziki na uimuaji wa vipaji hauwezi kuwa mkubwa. 

Sasa yawezekana mtu anatamani kusolo lakini kumbe aina ile ya mziki haifanani na yeye sasa hapo huwezi pata nafasi. Lakini utakutana na mtu amepata kanafasi ka kusolo na hajui kwamba hajui na hajui kwamba kwenye hicho kikundi yeye ni wa afadhali tu basi ndio utakutana na kiburi cha ajabu. Kiburi ni uthibitisho wa mtu asiye na kipaji na ambaye amepewa tu nafasi kwa kutengenezwa. Lakini inatokea kwa bahati tu mwalimu anakuangalia na anakupa nafasi usidhani kwamba unajua ila huwa ni bahati tu na kiburi chako ndio huwa ujinga wako.

Mimi mara nyingi sana naongea na wanafunzi wenye vipaji vizuri na tunaelewana sana. Wengi hupenda kunipa changamoto mpya na kunitambishia uwezo wao tukiwa mazoezini. lakini jukwaani tunaheshimiana sana na kupeana maelekezo kwa usahihi sana.

Hata studio nikifanya kazi na wenye vipaji wananiheshimu sana lakini sasa mara nyingi vipaji nilivyovitengeneza ndio wanaongoza kuniona nakosea na wangependa wanikosoe mara nyingi. wao hawapendi upendeleo wliofanyiwa wao wafanyiwe na watu wengine pia. Wangependa wawe wao milele. Na hapa ndipo ugomvi huwa umepata njia ya kujitambulisha.
itaendelea...................................................


Itaendelea......
Mwalimu na mtayarishaji wa muziki wa injili Tanzania
John Mtangoo 2016


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.