AUNTY EZEKIEL AMKABIDHI MWANAYE KWA YESU NA KUKIRI BILA YEYE ASINGEMPATA

Aunty Ezekiel na binti yake ©Ayo TV
Yawezekana kwa waliowengi taarifa hii ikawa haiwapendezi kwakuwa wanadamu tumekuwa na kawaida ya kuhukumu na kujiona wasafi sana kuliko wengine. Kuna jambo ambalo kama GK imeliona na kufurahishwa nalo sana; pale msanii maarufu wa maigizo nchini Aunty Ezekiel alipoamua kuweka bayana namna gani Yesu alivyo muhimu katika maisha yake hasa ya mtoto wake Cookie ambaye ametimiza mwaka mmoja hivi majuzi.

Katika video iliyotolewa na mtandao wa MillardAyo mwigizaji huyo alikuwa akitoa shukrani kwa Mungu na kumkabidhi mtoto wake huyo kwa Mungu kwa kubatizwa siku hiyo ya kuadhimisha mwaka mmoja (dhehebu lake linaruhusu mtoto kubatizwa...) na kwamba amesema bila Mungu asingepata mtoto huyo hali iliyofanya wahudhuriaji kupiga makofi kuonyesha kukubaliana naye.

GK imefurahishwa namna ambavyo msanii huyu alivyoweza kuonyesha kukubali kwamba bila Kristo yeye si lolote... kikubwa GK inamuombea kwamba apate kutengeneza na Mungu pale ambapo anajua hayuko sawa.

Aunty Mungu anakupenda, tunazidi kukuombea kwamba Yesu asitajwe kinywani tu bali pia maisha yetu yote tumpe yeye atuongoze na kufanyika barua njema kwa wote wanaotuzunguka. Ubarikiwe

Mose Iyobo na familia yake ©Ayo TV


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.