CHAGUO LA GK: AFADHALI YESU KUTOKA KWA SIZE 8 REBORN

Size 8 Reborn ©Trending Post KE
Tunatumai u mzima mdau wa GK, nasi katika Chaguo letu wikii tunakueletea mwanamama kutoka Kenya, Linet Muraya maarufu kwa jina la Size 8 Reborn; ambaye anatukumbusha jambo moja kwamba hapa duniani tunaweza kusaka vyote (mali na fedha) na kuzipata bila ya kuridhika - kinachofuata ni kutaka kujilimbikizia zaidi na zaidi.

©Fb/Size 8 Reborn
Lakini pamoja na yote, furaha na amani vinatoka kwa Yesu mwenyewe, hivyo unaweza kuwa na mali nyingi lakini maisha yakawa ya mateso vilevile. Video hii iliyoandaliwa na kampuni ya True Defination Pictures inatukumbusha kwamba afadhali yeye aliye na Yesu, maana tunachothamini kumbe hakitufanyi kuwa na furaha.

Sikiliza kwa makini mistari na kisha utafakari upya maazimio yako kwa kila unachoamua kufanya.
Mistari ya kuimba naye;

ubeti wa kwanza
Nimepanda, nimeshuka, milima mabonde na mito nimevuka
Nimeoza, nimesota, nimekosa mpaka mpaka nimekopa
Nimeamini binadamu, ole wangu roho akanivunja
Niliambiwa nikakana, mimi mwenyewe nimekuja ona

kibwagizo
Tunachothamini hakitufanyi tufurahi
Ooh najiuiliza furaha yangu ni nani?

kiitikio
Afadhali Yesu, afadhali ye aliye na Yesu
Afadhali Yesu, afadhali ye aliye na Yesu
Afadhali Yesu, afadhali ye aliye na Yesu
Afadhali Yesu, afadhali ye aliye na Yesu

ubeti wa pili
Nimesaka-saka-saka mali sana, nikipata pata bado nataka more
Nimesaka-saka-saka pesa sana, nikipata pata bado nataka more
Makosa yangu na dhambi zangu, matendo yangu yale ninajuta
Umechukua umeondoa, ulisema hutayakumbuka

kibwagizo
Tunachothamini hakitufanyi tufurahi
Ooh najiuiliza furaha yangu ni nani?

kiitikio
Afadhali Yesu, afadhali ye aliye na Yesu
Afadhali Yesu, afadhali ye aliye na Yesu
Afadhali Yesu, afadhali ye aliye na Yesu
Afadhali Yesu, afadhali ye aliye na Yesu
***

Tunakutakia Jumapili yenye baraka tele.

Mistari kwa hisani ya GK | Uimbaji

Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.