CHAGUO LA GK NI KUTOKA KWA GWIJI LA MUZIKI BARANI AFRIKA


Leo chaguo la GK linaangukia nchini Zimbabwe ambako tunakutana na kundi maarufu kwasasa nchini humo liitwalo Zimpraise ambalo linaendesha shughuli zake kama kundi la Joyous Celebration nchini humo. Kupitia DVD yao mpya waliamua kumshirikisha mkongwe wa muziki Oliver Mtukudzi ambaye ana mchango mkubwa katika muziki wa nchi hiyo ya Zimbabwe.

Mtukudzi ana wimbo mfupi ambao anauita sala maalumu kwake kwenda kwa Mungu uitwao "Hear me Lord" ni wimbo mfupi wa maneno machache lakini mwimbaji ama mtunzi anasema maombi ni maombi haijalishi kama ni marefu au mafupi kikubwa ni kumaanisha kwa yale maneno yako. Mwimbaji huyo amesema wimbo huo umefanyika baraka kwake pia amekutana na Mungu kupitia wimbo huo.

Maneno ya wimbo huo ni machache kama ifuatavyo.....ila nimependa jinsi Zimpraise walivyoupiga


"Hear me Lord
Hear me I pray
Help me now, help me Lord
Help me Lord I'm feeling low"

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.