HATIMAYE KILIO CHA WANAMUZIKI AFRIKA YA KUSINI CHASIKIWA

Soweto Gospel Choir pamoja na Ladysmith Black Mambazo.
Hatimaye kiu na haja ya wanamuziki wa Afrika ya kusini kutaka redio na TV za nchi yao kupiga zaidi nyimbo zao badala ya zile za kimataifa limekubaliwa na shirika la utangazaji la nchi hiyo (SABC) baada ya kikao cha wawakilishi kutoka kwa umoja wa waimbaji na wanamuziki nchini humo kilichofanyika jana.

Katika barua iliyotolewa na shirika hilo, imesema kuanzia leo tarehe 12 May 2016 radio zipatazo 18 zilizochini ya shirika hilo, litatoa kipaumbele katika kupiga nyimbo za wakongwe na wale wanaochipukia kwa asilimia 90 ili kuendeleza na kudumisha utamaduni wao wa Afrika ya kusini.Aidha hatua ambayo GK ikaamua kuandika habari hii ni pale ambapo iliwahi kupata moja ya malalamiko ya mmoja wa wanamuziki nchini humo aliyesema radio za biashara ziliruhusiwa kwa mujibu wa sheria kupiga nyimbo za waimbaji wa nchi hiyo kwa asilimia 25 huku zile za serikali chini ya SABC wakitakiwa wapige kwa asilimia 40 kitu ambacho mlalamikaji huyo alilalamika na kutaka hali hiyo iangaliwe tena kwakuwa haiwasaidii waimbaji wa nchi hiyo badala yake waimbaji wa kimataifa.

Angalia malalamiko ya mwanamuziki huyo aliyotoa mapema mwezi November mwaka jana


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.