HIS TOUCH THROUGH WORSHIP, MEI 22 EAGT MAJENGO MOSHI

Hakuna awezaye kupinga, ya kwamba kusifu na kuabudu kuna nguvu. Hakuna awezaye kusema muziki ni jambo jepesi. Ala zake pekee zinaweza kufikisha ujumbe na hata kubadili hisia zilizokuwa zinamtatiza kiumbe yeyote.

Kwa muktadha huo, Jiji la Moshi litashuhudia masaa matatu yaliyo timilifu katika kumuabudu Mungu, kumrudishia sifa na utukufu, pamoja na kukiri ya kwamba hakuna Mungu mwingine zaidi ya Baba yetu, Jehova.


Tukio hili litafanyika ndani ya EAGT Mejengo, Jijini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro kuanzia saa tisa mchana hadi saa kumi na mbili. Ukichelewa ukapitwa, mikono tunanawa. Team GK itakuwepo.
Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.